Kwenye Kitabu cha Mithali kuna Mstari unasema Hasira Hukaa Kifuani kwa mpumbavu. Maana yake ni nini Hasa? Maamuzi yeyote yanayofanywa kwa hasira hayajawahi kuwa maamuzi bora hata siku moja. Maneno yote yanayozungumzwa na mtu mwenye hasira hayajawahi kuwa yenye busara hata siku moja.

Hasira ni hisia ambazo zinakuja juu sana pale mtu anapoaibishwa, au kufanyiwa jambo asilolipenda. Hasira humtokea mtu yeyote lakini ni wachache wanaoweza kuziongoza hasira zao.

Mara zote angalia yale mambo uliyofanya ukiwa na hasira mara zote umekuja kujutia sana. Hasira zinapokwisha na unapopata akili zako sawasawa ndipo unatambua kwamba maamuzi ulofanya yalikuwa ya kipumbavu.

Hasira zikiisha ndio unajiona jinsi gani ulivyojidhalilisha kwa kuporomosha matusi au kujaribu kupigana mbele za watu.

Hasira zikiisha unapata akili zako sawa sawa maana yake ni kwamba wakati una hasira akili yako yaani ufahamu wako unakuwa haufanyi kazi sawasawa.
Kuna wengine hasira zao huwapeleka kuharibu vitu mbalimbali vitakavyokuwa mbele yao. Ila yoote ni yaleyale kwamba hasira hukaa kifuani kwa mpumbavu.

Ukijibu kwa hasira na jazba huwezi kujibu sawasawa hata siku moja.
Kama unakumbuka ulipokuwa mdogo ukipata hasira sana unaambiwa ukanywe maji au unawe uso.

Hii ni njia ya kwanza ya kushusha hisia zako za hasira. Kama unafikiri una hasira sana kiasi kwamba huwezi kuvumilia tafuta maji ya baridi kunywa. Maji yatakufanya upumue na uweze kushusha hisia zako za hasira.

Njia ya pili ni ya kupumua. Unapokutana na hali yeyote iliyokufanya ukapatwa na hasira sana. Unaweza kushusha hasira zako kwa kuvuta pumzi kubwa ndani na kupumua taratibu kwa kurudia zoezi hilo mara tatu utakuwa umepunguza kabisa hasira zako.

Hasira ni hasara unaweza kuua, Kuharibu mali, Kuharibu sifa yako, Kujiabisha Zaidi, kuonyesha ulivyo mdogo kiufahamu na mengine mengi sana.Karibu sana, Soma Kitabu Changu Siri 7 za Kuwa Hai Leo Chukua Oda yako kwa 0654726668
Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255654726668

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading