Mafanikio ni safari na safari yeyote ina changamoto zake. Usione wanaopanda ndege ufikiri huwa nyakati zote ni furaha tu. Kuna wakati ndege hupata misukosuko angani pia.
Misukosuko yeyote unayopitia tambua ni safari huwa zipo hivyo. Ukifika wakati wa kula safarini wewe kula, Ukifika wakati mnatakiwa mpumzike pumzika. Bahati mbaya sana hili gari la Mafanikio unaendesha mwenyewe na kila mmoja ana usafiri wake. Kila mmoja ana sehemu yake anafika.
Ni muhimu sana kufurahia wakati wa safari hii ya Mafanikio. Tulipotoka haturudi tena. Kuna vitu vikishapita hutaviona tena. Kama bahati mbaya ulikua umelala ndo hivyo tena usubirie vingine vilivyoko mbele ya safari.
Cha Kujifunza:
Hakuna aliyewahi kuahirisha safari Kwasababu ya misukosuko anayopitia njiani. Yaani wewe unatoka Dar unaenda Mwanza halafu Kwasababu tu ya changamoto za barabarani useme sasa mimi nitabaki Dodoma sisafiri tena. Haiwezekani zaidi utakachofanya ni kupumzika Dodoma kisha uendelee na safari yako. Mwisho wa safari yetu ni kifo. Yaani kama bado una uwezo wa kufanya kitu kwa sasa haijalishi una umri mkubwa kiasi gani wewe fanya.
Furahia Safari, Misukosuko ni Sehemu ya Safari.
Jacob Mushi.
INUKA UANGAZE.
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com & www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.