Ndugu yangu asikwambie mtu kitu cha muhimu kuliko vyote ni afya yako. Unajua kwanini? Kama afya yako ni mbovu hata upewe kitu gani kizuri huwezi kukifurahia hata kidogo.

Kama afya yako ni mbovu hata ukipanda ndege nzuri kuliko zote huku duniani huwezi kufurahia kama mwili wako una maradhi.

Dalai Lama aliwahi kusema maneno haya “Man surprised me most about humanity. Because he sacrifices his health in order to make money.Then he sacrifices money to recuperate his health. And then he is so anxious about the future that he does not enjoy the present; the result being that he does not live in the present or the future; he lives as if he is never going to die, and then dies having never really lived.”


“Watu wananishangaza sana juu ya ubinadamu wao. Kwasababu anatoa sadaka afya yake ili atengeneze pesa, halafu anakuja kutoa pesa zake zote kwa ajili ya kutengeneza afya alioiharibu wakati akizitafuta pesa.” (Tafsiri Isiyo Kamili)


Inawezekana na wewe ni mmoja wa watu wengi wanaosahau kabisa kujali afya zao wanadhani wakishapata pesa sasa ndio wataanza kwenda hospitali kujitibu vizuri. Ondoa kabisa mawazo ya aina hiyo mwanamafanikio mwenzangu. Ni muhimu sana uwe unakwenda hospitali kucheki afya yako mara kwa mara. Ni muhimu sana ujali mwili wako kwa kula vyakula bora, fanya mazoezi, chukua tahadhari pale unapokutana na hatari.

Ukipata kila kitu unachokitafuta utajiri wote, umaarufu wote mali zote halafu ukakosa afya bora, huwezi kuwa na furaha kabisa kamwe usisahau kuweka Afya katika mpango wako wa kila siku. 

Magonjwa yanaua watu wengi sana wengine wanaondoka ndoto zao hazijatimia. Usikubali uwe mmoja wao. Usikubali kuuza mwili wako kwa ajili ya shida ya siku moja.

Una shida ya kupendeza sana ndio lakini afya yako ni muhimu sana kuliko kupendeza kwa nje. Kuna mabinti wanafikia kujiuza eti ili apate pesa ya kununua nguo nzuri. Unapata hiyo nguo nzuri na mwili wako umepata maradhi ya kudumu. Nguo itachakaa maradhi yakuua.


Kuna wengine wakishapata pesa kiasi fulani ndio wanasahau kabisa kufanya mazoezi kula vyakula bora na magonjwa yanawavamia unasikia huyu kafa na presha mara kisukari. Usikubali kabisa kuisahau afya yako.

Mwili wako ndio unafikiria, unautumia kuchukua hatua mbalimbali za mafanikio upatie uangalizi mzuri.

Soma kitabu Changu Kinaitwa Siri 7 za Kuwa Hai Leo. Chukua oda yako 0654726668
 Karibu Sana. 
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading