HATUA YA 51: Kuna Tatizo Una Tatua?

jacobmushi
2 Min Read
Katika zama hizi za sasa kila unachokifanya kuna mwingine anakifanya. Kama hakuna basi muda si mrefu wataanza kukifanya hasa wakiona kuna matunda. Ni muhimu sana kujua sehemu uliyopo kama ni sahihi kwako au lah!

Unaweza kukutana na watu wengi ambao watakuonyesha vitu vingine vizuri vya kufanya zaidi ya kile unachokifanya sasa hivi. Watakuonyesha ni jinsi gani unaweza kunufaika zaidi kuliko hapo ulipo sasa hivi. Sio vibaya ukawasikiliza na kujifunza juu ya wanachokueleza lakini ni muhimu sana kuwa makini unapofanya maamuzi.

Kabla hujaacha unachokifanya sasa kwasababu tu umeonyeshwa kingine kinacholipa zaidi lazima ujiulize maswali ya msingi ili usije kuondoka ukapotea.

Hapo ulipo sasa ni Tatizo gani unalitatua?

Ni tatizo gani hasa unalolitatua sasa kwenye kile unachokifanya? Tatizo hili ndio la msingi sana kwako na wewe uweze kujua unawasaidiaje hawa wenye tatizo lenyewe na kwa wingi kiasi gani ili upate kuongezeka.

Kitu gani kinakutofautisha na wengine?

Ni kitu gani ufanye ili uwavute wateja wengi zaidi ya ulio nao sasa?

Usipojiuliza maswali huwezi kupata majibu. Kama kuna tatizo lipo ndani ya biashara yako na linafanya isikue ni wakati wako sasa wa kulitafutia suluhisho.


Kabla hujaacha tu na kuanza biashara mpya lazima pia utambue ni sababu gani inafanya biashara yako ya mwanzo isikue? Kama sababu ni wewe hata ukianza biashara mpya na nzuri kiasi gani haitakuwa utakwama njiani.
Kabla hujaacha hakikisha umejua kabisa tatizo ni lipi ili usije kurudia makosa yale yale kwenye biashara yako mpya. Matatizo mengi tunayasabisha sisi wenyewe kutokana na uzembe ambao tunaleta kwenye biashara. Watu tunaowapa nafasi za kusimamia wanashindwa kuzisimamia sawasawa.

Chukua Hatua Mapema.
Karibu Sana.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading