Mawazo hasi ni mojawapo ya vitu ambavyo vinaharibu Maisha ya watu wengi kwa namna mbalimbali. Mawazo hasi mara nyingi humjia mtu pale anapokata tamaa, anapopitia magumu, au anapokutana na vikwazo vya namna mbalimbali kwenye kile anachokifanya.

Mawazo hasi yameharibu mahusiano mengi sana. Mawazo hasi huanza kuja pale mtu anapokuwa amepata hisia kwamba mwenzake anamsaliti. Mawazo hasi huchipuka kidogo kidogo hadi kusababisha mfarakano kwenye mahusiano mwishowe huvunjika. Ni kweli kuna mawazo hasi na ukweli halisi. Lakini mahusiano mengi yanavunjika kwasababu ya mawazo hasi.

Ukiona mtu ana chuki na wewe chuki hiyo ilianzia kwa kuwaza hasi juu yako. Ukiona mtu amefikia kuchukua hatua ya kufanya mauaji anakuwa anaendeshwa na fikra hasi juu ya mtu yule anaetaka kumuua.

Kuna maneno yanasema kwamba ukitaka kuona vitu vizuri juu ya mtu utaviona tu. Na ukitaka pia kuona mabaya ya mtu utayaona sana. Mawazo hasi yanakuja katika fikra zetu kwasababu tumeamua kuyapokea. Tunafikiri vibaya juu ya wengine kwasababu tuliamua hivyo. Ukitaka kupata mazuri juu ya mtu kuwa chanya juu yake chochote anachokifanya hata kama hakijakufurahisha jaribu kutumia lugha ambayo itamfanya akuelewe bila kuchukia.

Mawazo hasi yanasababisha watu wengi kufikia hatua ya kujiua. Mtu anapokuwa na fikra hasi juu ya Maisha yake na akakosa mtu yeyote wa kumtia moyo mwisho wa siku hukata tamaa na kufikia hatua ya kujiua.

Mawazo hasi husababisha watu washindwe kuona fursa. Unapotembelea eneo ambalo ni jipya kwako na wewe una fikra hasi hutaweza kuona fursa. Utaishia kukosoa na kisha utaondoka zako.

Unapokutana na mtu anaefanya jambo ambalo unalifanya wewe kama una fikra hasi mara nyingi utashindwa kumkubali.

Watu wengi wameshindwa kutoka sehemu walizopo kwasababu ya fikra hasi walizonazo juu ya mambo mbalimbali, biashara, mahusiano, dini zao, na watu wanaowazunguka. Ukiweza kufikiri chanya kwenye kila jambo mafanikio yatakufuata. Kuna njia zitaanza kufunguka zenyewe.

Soma: KunaTatizo Unatatua?

Ngoja nikwambie kitu hivi unajua kwamba ukimuajiri mtu asimamie kazi yako halafu yule mtu akaja kutambua kwamba wewe humwamini hata kidogo na unafikiri ni mwizi. Unajua kwamba kuna uwezekano mkubwa yule mtu akaanza kufanya yale uliyokuwa unawaza juu yake? (Kama na yeye hafikiri chanya)

Fikiri chanya wawazie wengine mazuri. Maisha yako yatakuwa na furaha.

Jiunge na Mtandao wetu uwe unapokea makala hizi moja kwa moja kwenye email yako. Mwishoni mwa makala hii kuna sehemu ya kuweka email na chini yake pameandikwa Subsrcibe. Weka email kisha Bonyeza Subscribe.

Ubarikiwe sana,

Rafiki Yako, Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/kocha

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading