Kwenye Kitabu Cha Biblia Musa alipokuwa anawatoa wana wa Israel kutoka Misri kuelekea Kaanani, walikwama kwenye bahari ya Shamu.

Wana wa Israel kama kawaida yao wakaanza kumlalamikia Musa waliona hakuna namna kabisa ya kuendelea mbele tena. Waliyaona maji kama kikwazo kwao hivyo wakakata tamaa ya safari yao.

Musa nay eye hakuchelewa alimwendea Mungu aliemuagiza awatoe Misri akamwuliza afanye nini! Mungu alimuuliza Musa una nini mkononi mwako? Musa alijibu ana Fimbo. Tukumbuke Fimbo hii ilishatumika huko nyuma kufanya miujiza mbalimbali kama kubadilika na kuwa nyoka kisha ikawameza wale nyoka wa waganga.

Musa alisahau kabisa kwamba alikuwa na kitu mkononi mwake ambacho kingweza kumsaidia kuvuka Bahari iliyo mbele yake.

Inawezekana hata wewe unapitia changamoto kubwa sana kwenye Maisha yako kwa sasa. Inawezekana ni madeni yamekuwa mengi sana hata umefikia kukata tamaa. Inawezekana pia unachokifanya hakionyeshi matokeo yeyote ya kule unakotaka kulekea.

Inawezekana pia hujaelewa mpaka sasa ufanye nini ili ndoto yako itimie. Leo nataka kukwambia kwamba una nafasi ya kutoka hapo ulipo.

Una nini mkononi mwako?

Hakuna aliesaidiwa bila kuwa na kitu mkononi au nyumbani kwake. Hakuna muujiza uliowahi kutendeka bila kuunganishwa na kitu Fulani ambacho anacho yule anaetaka kutendewa muujiza. Hivyo ni muhimu sana ukatambua ni nini unacho mkononi?

Kile ulichonacho ndio tunakwenda kukitumia kuanza safari au kuendelea na safari pale ulipokwama. Haijalishi ni kwa kiasi gani gani umekaa hapo ulipo, jiulize tu una kitu ganu mkononi mwako?

Labda una Simu nzuri sana ya ghali, una Computer nzuri sana unaitumia kuangalia picha za maigizo hujajua matumizi yake ili utimize ndoto yako. Inawezekana simu yako waitumia vyema sana kuchati tu lakini hujajua kwamba inaweza kutumika kama njia ya kuingiza pesa.

Soma: Unamhitaji Mtu Huyu

Una nini mkononi mwako? Ulicho nacho kwa namna moja au nyingine kinakuwa kinaendana na kile unachotaka kukifanya. Inawezekana unakipaji kizuri sana lakini hujajua ni jinsi gani unatakiwa uanze.

Una nini mkononi mwako?

Jiulize leo una nini mkononi? Unatumiaje ulichonacho kufikia ndoto zako?

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author | Trainer | Entrepreneur

Simu: 0654 726 668 |0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Facebook:  Jacob Mushi 

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading