Kuna wakati mtu unapitia changamoto hadi unajiuliza hivi nafanya kitu sahihi kweli?
Unapitia magumu hadi unafikiri labda unakoelekea siko kwenyewe.

Leo nataka nikwambie haijalishi ni changamoto gani unapitia, haijalishi ni ugumu gani unapitia. Kama unachokifanya ndio kinaupa moyo wako utoshelevu kuliko vitu vingine vyovyote endelea kufanya upo sehemu sahihi.
Kama unachokifanya ndio kinakupa furaha ya kweli hapo upo sehemu sahihi.

Haijalishi unaona mbele au huoni. Kuna wakati wa kupanda milima hivyo hatuoni kule mbele tunapoelekea vizuri. Hivyo mlima usiwe sababu ya wewe kuacha kuendelea na safari yako.

Kama unachokifanya upo tayari kukifanya hata bure upo tayari kufanya haijalishi wingi wa changamoto. Hapo ni sehemu sahihi upo.

Kama unachokifanya wewe unapenda tu na kufurahia wakati wa mazuri pekee kuna walakini. Kama unachokifanya hakikupi nafasi ya kukua na kuongezeka haijalishi unapata pesa kiasi gani upo sehemu ambayo inatia mashaka.

Tofautisha sehemu ambayo inakupa faraja ya muda (comfort zone) na sehemu ambayo inakupa utimilifu moyo.

Fanya kwa bidii, tafuta maarifa zaidi ili uweze kusonga mbele.
Unaweza kuifikia ndoto yako maana upo sehemu sahihi.

Soma: Una Nini Mkononi?

Upo sehemu sahihi na wakati sahihi kabisa kupata changamoto unazopitia sasa hivi.
Itazame ndoto yako.

Karibu sana.

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading