Inawezakana ulikua hujatambua hili na ukajikuta unapoteza nguvu yako ya kwenda mbele zaidi.
Mafanikio sio kitu ambacho unataka kukikamilisha bali ni hatua ambazo unazifikia kila siku.

Kadiri unavyoweza kupiga hatua ndio tunahesabu hayo ni mafanikio. Kama utachanganya katika ufahamu wako mafanikio na hatma utajikuta unakosa furaha na wakati mwingine kukata tamaa.

Rafiki yangu ngoja nikwambie ukishindwa kuelewa hivi, utajikuta unaumia moyo na kujiona wewe uko nyuma sana unapotazama vitu vya wenzako.
Mafanikio ni hatua au matokeo kidogo kidogo tunayopata kila siku. Matokeo haya yanapojumuishwa pamoja ndipo utaona mambo makubwa.

Rafiki kama wewe Unawaza kumiliki kampuni yenye mtaji wa milioni mia moja ili uwe nayo sasa hivi labda ukakope. Na ukienda kukopa lazima uanze kazi ya kurudisha kidogo kidogo hadi deni liishe.

Badala yake sasa unaweza kuanza wewe mwenyewe. Ukajikusanya kidogo kidogo hadi ukaweza kufikia hiyo biashara yako kubwa.

Mti wa mwembe hasa hii ya kienyeji sio hii ya kisasa, hadi uanze kuzaa maembe inachukua muda mrefu sana. Lakini mti huu ukishakuwa tayari kuzaa unazaa hadi siku ya mwisho.
Wewe jiandae tu taratibu songa mbele hata kama huoni matokeo yeyote sasa hivi.

Tunaotesha mwembe leo lakini tunategemea matunda yake baada ya miaka mitano. Lakini hatuishii njiani na kusema huu mwembe haukui tu!

Usijilinganishe na mtu mwingine yeyote. Endelea kupiga hatua zako. Hata kama mnalingana elimu, umri na kingine chochote, kila mmoja ana njia zake za mafanikio.

Rafiki yangu usisahau kujifunza kila siku maana huu ndio msingi wa mafanikio.

Mafanikio makubwa yanaunganishwa na hatua ndogo ndogo tunazopiga kila siku.
Matokeo madogo madogo tunayopata kila siku ndio yanaleta mafanikio makubwa.

Soma: Kama Upo Hapa Upo sehemu Sahihi

Usikate tamaa wala kuishia njiani.

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading