Linalowezekana Kufanyika Leo Lisingoje Kesho. Pamoja na kwamba unakuwa na vipaumbele vyako vya maisha lakini siku zote linapojitokeza jambo ambalo linatakiwa kufanyika sasa hivi lifanye sasa hivi kwani kadiri unavyoahirisha ndio unajitengenezea mambo mengi huko baadae ya kufanya.

Kuna changamoto unapitia sasa hivi zinatokana na vitu ulivyovipuuzaga huko nyuma kwasababu zako binafsi. Kuna ugonjwa unaumwa sasa kwasababu ulitakiwa uanze kufanya mazoezi kipindi cha chuma ukaahirisha.

Nimekutana na watu wengi sana ambao wana katabia kakusema nikiwa tayri nitaanza. Nikiwa tayari nitakwambia, na hadi sasa hakuna aliechukua hatua.
Kama jambo una uhakika hutaki kulifanya amua moja kwa moja sifanyi kitu hiki, usilete sababu za kujipanga, mara nitakwambia, najikusanya na mengine mengi.

Anza kusoma sasa hivi, anza kufanya mazoezi sasa, anza kutengeneza baadae yako sasa hivi. Hakuna wakati mwingine ambao unadhani ni bora Zaidi ya sasa. Ukisema unasubiri upate pesa ni kwamba hata ukizipata mara nyingi unajisahau na kwenda kufanyia mambo mengine.

Nimekuwa na marafiki zangu ninawashirikisha fursa nzuri wanahamasika kweli lakini kwenye kuchukua hatua wanasema ngoja mwezi ujao. Mwezi ujao ukifika mtu anakwambia ooh nilipata ile pesa nikalipia madeni yote! Sasa unajiuliza huyu mtu si atakwenda kukopa tena kama amelipia madeni pesa yote?

Kadiri unavyoahirisha mambo ndio kadiri unavyoahirisha maisha yako. Kuna mambo ulitakiwa uyafanye sasa hivi usipoyafanya yatakuja kuwa changamoto kubwa sana kwako huko baadae. Yatakuja kuwa kikwazo kwa mambo mengine huko baadae.

Kuna watu wanasemaga ngoja nikajipange lakini hawajawahi kumaliza kujipanga hata siku moja. Kila kitu kizuri kinachokuja anahamasika na kuishi kusema ngoja nikajipange. Badala ya kusema unaenda kujipanga embu sema tatizo lako upatiwe suluhisho.
Kuna watu nikiwauliza hivi mlishamalizaga kujipanga tangu siku ile unashangaa kumbe hata jambo lenyewe hawajawahi kulifanyia kazi. Liliishia pale waliposema ngoja nikajipange.


Hakuna mtu mwingine anaetakiwa kujali na kufikiria maisha yako kwa nguvu sana Zaidi yako wewe.

Kama unawaza mtu ambae atakuja kuyabadilisha maisha yako nenda kamtazame kwenye kioo utamwona.

Jipatie nakala ya Kitabu changu Kiitwacho Siri 7 za Kuwa Hai Leo. Hapa Utatambua thamani ya uhai ulio nao sasa na jinsi ya kuutumia kuleta matokeo bora duniani nitumie ujumbe kwenye 0654726668

Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading