HATUA YA 6; Nidhamu

Nidhamu ndio kitu cha muhimu sana katika safari yetu ya Mafanikio. Nidhamu ni pale unapoamua kufanya kitu iwe unataka au hutaki. Kama umesema utasoma vitabu viwili kwa mwezi usome kwa namna yeyote ile.
Nidhamu ndio inaweza kukufanya ujijengee tabia mbalimbali nzuri za Mafanikio. Kama mimi nilipoamua kuandika makala hizi za kukutia moyo na kukushauri. Haijalishi nipo kwenye hali gani lakini ni lazima niandike. Wakati Mwingine unakuwa umechoka lakini hakuna namna nyingine lazima ufanye.
Kitu kinachowafanya wengi waishie njiani kwenye vitu wanavyovianza ni kukosa Nidhamu. Nidhamu imegawanyika kwenye vitu vingi sana.
Unaweza kuwa na Nidhamu kwenye matumizi ya pesa.
Nidhamu kwenye utunzaji wa muda wako.
Nidhamu kwenye Kusoma.
Nidhamu kwenye kufanya mambo uliyojiwekea kwenye ratiba yako ya kila siku.
Nidhamu ya kuamka asubuhi na mapema.
Nidhamu ya kukaa mbali na mitandao ya kijamii.
Embu tazama hayo hapo juu na uangalie ni namna gani unaweza kuyaingiza kwenye maisha yako ili ujijengee tabia bora za Mafanikio.
Hakuna kingine kinachowaangusha watu zaidi ya Nidhamu. Hakuna kinachowafanya watu washindwe biashara kama ukosefu wa Nidhamu.
Naamini Hatua hii hutairuka.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com,www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Posted

in

by

Tags:

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *