HATUA YA 60: Kufanya Kwa Mazoea.

jacobmushi
3 Min Read
Inawezekana unafanya vizuri sana lakini hupati matokeo mapya mambo yanakuwa yale yale kwasababu unafanya kwa mazoea.

“Hatufanyi vitu vya tofauti, tunafanya vitu vilevile lakini kwa tofauti”


Kama unachokifanya kuna mtu mwingine anaweza kukifanya kabisa yaani sawa sawa na wewe ujiangalie vizuri sana.

Inawezekana biashara moja wakaifanya watu wengi na baadhi yao wakapata matokeo bora yaani mafanikio na wengine wasione mabadiliko yeyote hii inasababishwa na ufanyaji.

Kama hupati matokeo angalia namna unavyofanya, wenzako waliofanikiwa wanafanyaje? Kuna kitu gani ambacho kinakutofautisha na wengine?
Utofauti wako ndio unaleta maana ya kile unachokifanya. Kama hakuna tofauti unachokifanya kinakuwa cha kawaida tu.

Usikubali kufanya vitu kwa mazoea kabisa. Kama unataka mafanikio anza kubadilika. Huu ni mwezi wa pili wa mwaka huu na mara nyingi kadiri tunavyosonga mbele kuingia katikati yam waka ndipo watu huanza kuacha yale waliyosema watafanya.

Inawezekana na wewe umeshaanza kurudia hali yako ya mazoea. Hata kusoma hutaki tena. Kununua kitabu unaona ngumu sana. Yaani unataka vitu virahisi tu uletewe hapo mdomoni ule.

Mafanikio yanahitaji watu walioamua kufanya vitu vya tofauti.
Aliegundua simu janja (smartphone) sio mwanzilishi halisi wa simu bali ni mojawapo ya watu waliofikiria kwa tofauti na wakaleta mapinduzi haya tunayoyaona. Sasa ni kazi kwako pia kuangalia hapo ulipo na kile unachokifanya ni kwa njia gani unaweza kufanya kwa tofauti na ukaleta mapinduzi?
Mazoea yameharibu mahusiano na ndoa nyingi sana pale mtu anapoona sasa tayari nimeshampata hawezi kuniacha tena na kisha akaanza kusahau yale ambayo alikua anayafanya yakasababisha akaoa au akaolewa. Inawezekana mtu alikubali kuwa na wewe kwasababu ulikua una vitu Fulani unafanya anafurahi sasa baada ya kuwa pamoja umejisahau hufanyi tena yale uliyoyafanya mwanzoni.

Mazoea yameua biashara nyingi sana, mtu anakaa dukani anasubiria mteja aje anunue. Dunia ya sasa inabadilikka umejipangaje kumfata mteja kule alipo? Kuna wageni wangapi wanaingia kwenye mji wako kila siku? Hawa wateja ungeweza kuwajulisha kabla hawajaja kwamba una duka la kitu Fulani hapo ulipo. Wakija wanakuja kununua. Endelea kushangaa tu sasa hivi dunia inabadilika acha mazoea. Haijalishi biashara ni ndogo kiasi gani kama una lengo la kufikia mafanikio makubwa acha kufanya kwa mazoea badilika.

MAISHA YA MAZOEA NI MABAYA SANA NA YANAWAFANYA WATU WAWE WA KAWAIDA ACHANA NAYO HARAKA SANA.

Jiandae Kupata Kitabu Kiitwacho Siri 7 za Kuwa Hai Leo. Bado Muda Mchache Kitakuwa Mikononi mwako. Weka oda kwa 0654726668

Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading