Vile ulivyo sasa au kile kinachoendelea kwenye maisha yako sasa hivi kwa namna moja ama nyingine ulichagua mwenyewe. Kuna uchaguzi ulifanya na ukakuletea matokeo unayopata sasa hivi.

Ulichagua kutokuwa mwaminifu ndio maana mahusiano yako na mwenzako yakavunjika.

Ulichagua kutokusoma vitabu ndio maana huna maarifa ya kutosha juu ya kile unachokifanya.

Ulichagua kwa namna moja ama nyingine kupata ugumu unaoupitia sasa hivi. Kama umeugua magonjwa uliyonayo sasa kuna namna ulichagua na ukajikuta kwenye hali hiyo.

Una uzito au unene uliopitiliza ulichagua mwenyewe kula vyakula visivyo na afya kwenye mwili wako.

Umekuwa na madeni mengi kwasababu ulichagua kutokuwa na nidhamu ya pesa wala huweki akiba yeyote.

Umekuwa mtumwa na unateseka sana ndani kwasababu ya aina ya maisha ulochagua kuishi yanakulazimisha uigize, badala ya kuishi maisha ya uhalisia umechagua kuwaridhisha wengine.

Hakuna mtu mwingine anaekuchagulia mambo baadhi niliyotaja hapo juu kila moja unakuwa umefanya mwenyewe uchaguzi huo.

Maisha yako hayasogei mbele kwasababu umechagua kulalamika, kulaumu na mtu wa kumbebesha matatizo yako na ukasahau kuchukua hatua.
Maisha yako yataendelea kuwa mabaya Zaidi kama hutatambua namna ya kufanya uchaguzi bora ili uweze kufikia mafanikio yako.

Kama hujafanya uchaguzi wowote unapaswa uchekeche kwenye akili yako faida na hasara za uchaguzi unaofanya.


Unayo nafasi ya kufanya uchaguzi tena sasa wa kukuondoa kwenye vifungo ulivyonavyo na ukaanza kushi maisha unayoyataka sasa.

Unaweza kuamua kubakia hapo hapo ulipo kama hutafanya uchaguzi sahihi wa kuondoka kwenye hali uliyonayo.

Kumbuka: MAISHA NI YAKO, CHOCHOTE UNACHOKIFANYA KINALETA MANUFAA AU HASARA KWENYE MAISHA YAKO. UKICHAGUA KUWA MZEMBE MAISHA YAKO YATAKUWA YA HOVYO. UKICHAGUA KUWARIDHISHA WENGINE MAISHA YAKO YATAKUWA YA KITUMWA.

FANYA UCHAGUZI SAHIHI UISHI MAISHA BORA.

Weka Oda yako mapema ujipatie Kitabu Kiitwacho Siri 7 za Kuwa Hai Leo namba 0654726668

Your Partner in Success
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading