HATUA YA 63: Kuna Mtu Alifanya…..

jacobmushi
2 Min Read
Chochote unachokifurahia hapa duniani ambacho sio cha asili, ni matokeo ya binadamu mwenzako aliefanya kazi kwa bidii.

Kila siku kuna watu wanafikiri ni kwa jinsi gani waendelee kurahisisha maisha yetu kwa kupitia ugunduzi wa aina mbalimbali.

Kazi unayoifurahia sasa hivi na mshahara mzuri unaopokea kuna mtu alifanya kazi kwa bidii kukuza hiyo kampuni hadi wewe leo hii unaajiriwa.
Mawasiliano tunayotumia sasa hivi kwa urahisi sana tunaweza kuwasiliana kwa karibu Zaidi popote duniani kuna mtu alifanya kazi hadi tunaona matokeo haya.

Embu jiulize sasa hivi kwenye dunia hii kuna binadamu wangapi wanaofurahia kazi yako?

Kadiri watu wengi wanavyofurahia kile ulichokifanyia kazi kwa bidii ndio mafanikio yako yanakuwa makubwa sana.

Kitu ambacho unatakiwa ujue ni kitu gani hasa ufanye ili uguse maisha ya watu wengi sana kupitia hicho na hapo ndipo yalipo mafanikio yako.
Kitu cha pekee unachotakiwa kutambua ni kwamba kila mmoja wetu amezaliwa na zawadi ndani yake ambayo akiweza kuitumia vyema anaweza kufikia watu wengi sana kupitia zawadi hiyo.

Hakuna mtu aliezaliwa na kitu kwa ajili yake yeye, kila mmoja amezaliwa na kitu ndani yake kwa ajili ya wengine. Hivyo ukiweza kutumia kitu hicho kwa wengi Zaidi hapo ndipo penye mafanikio yako.

Ni kazi kwako sasa usiishie kuwa mtumiaji pekee bali na wewe ujue ni kwa namna gani unaweza kufanya kazi kwa bidii na wewe siku moja watu waseme na watumie kile ambacho umekifanyia kazi kwa bidii.

Kitu cha kufanya ni wewe ugundue upo duniani kwa ajili ya kufanya nini. Kitumie kitu hicho kuwagusa watu wengi Zaidi na hapo ndipo penye mafanikio yako.

Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading