Katika maisha tunafanya mambo mengi sana pamoja na maamuzi mbalimbali.  

Kitu kimoja ambacho huwa tunakosea ni kuwalazimisha watu watuelewe.   Mara nyingine unaweza kujikuta unashindwa kufanya mambo fulani kwasababu unahofia watakuelewaje.  

Leo nataka utambue kwamba huwezi kumridhisha kila mtu. Huwezi kumfanya kila mmoja akuelewe. Wakukuelewa watakuelewa tu. Ambao wataona makosa wapo wengi sana.  

Naomba utambue kwamba jambo lolote unalofanya kila mtu anaelewa kutokana na mtazamo wake ulivyo. Na mtazamo wake ndio unamfanya apate tafsiri fulani kulingana na jambo lenyewe.  

Binti ambaye ameumizwa sana na mahusiano akitokea mwanaume ambaye ana mapenzi ya kweli akaanza kwa maneno yale yale ya wengine, binti atatafsiri kwamba ndio wale wale hawa.

Kumbe kijana wa watu amemaanisha.   Kijana kama amezoea kuona mabinti wote wana tabia Fulani anaona kila anaekutana nae ni walewale.  

Lakini ukweli unabaki kwamba maana halisi na ukweli anao yule aliehusika.   Hivyo ni muhimu sana ukatambua hivyo ili usijikute unatumia nguvu nyingi kuwalazimisha wengine wakuelewe.  

Watu watakuelewe jinsi walivyotafsiri na sio jinsi wewe ulivyomaanisha.   Fanya kile moyo wako unachopenda na utawavuta watu wanaofanana na wewe.  

Karibu sana.  

Jacob Mushi

Entrepreneur & Author

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading