HATUA YA 66: Hivi ndio vinakukwamisha…

jacobmushi
2 Min Read

Haya ni baadhi ya mambo yanayokukwamisha kila siku na kukufanya ushindwe kusonga mbele.  

Kufikiri Unajua Kila Kitu.

Pale tu utakapoanza kujiona wewe ni mjuzi wa mambo na huwezi kujifunza tena kwa wengine hapo ndipo waanza kupotea. Haijalishi una mafanikio kiasi gani au umefikia kiwango gani, kujifunza ni kila siku. Unaweza kujifunza kwa kila mtu haijalishi amekupita kimafanikio au yupo chini yako. Kila unayekutana nae ana kitu ambacho ungeweza kujifunza kwake.  

Kujiona Wewe Huwezi.

Kuna tofauti ya Kufikiri unajua kila kitu na kujiamini kama tulivyoona hapo juu kufikiri kwamba wewe unajua kila kitu na hakuna wa kukufundisha au watu walioko chini yako kimafanikio huwezi kujifunza chochote kwao. Kujiona kwamba huwezi ni pale unajiona huna thamani kabisa na huwezi kutoka hapo ulipo.

Hali hii imekuwa ni sababu kubwa inayowarudisha watu wengi sana kwasababu hawachukui hatua yeyote. Jiamini kwamba unaweza na anza kutumia uwezo ulionao kuleta mabadiliko. Mabadiliko kidogo kidogo kila siku ndio yanaleta matokeo makubwa.  

Kulalamika.

Kama utaendelea kulalamika na kutoa sababu nyingi juu ya wewe kuwepo hapo ulipo siku zote haziwezi kukusaidia. Acha kutoa sababu chukua hatua. Acha kusema kwanini haiwezekani tafuta namna ya kuwezekana. Fanya mpango utoke hapo ulipo.  

Jacob Mushi

Entrepreneur & Author

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
1 Comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading