HATUA YA 67: Leo Unafanya Nini?

Kila siku ni siku mpya kwa ajili ya kutengeneza picha nzuri kwa ajili ya maisha yetu ya baadae. Hivyo siku inapokuja mpya ni nafasi kwako wewe kufanya vyema ili kujitengenezea matokeo mazuri siku za mbeleni.    

Ukweli ni kwamba tunaishi leo kila siku ila ili ufikie zile ndoto zako lazima ujue namna ya kufanya kidogo kidogo kila siku hadi picha yako kubwa ikamilike.   Kama siku inapita na hakuna unachokifanya unajitengenezea hatari kubwa sana kwenye maisha yako ya baadae.

Hii ni kwasababu matokeo unayoyapata sasa hivi yanaletwa na vitu ulivyokuwa unavifanya siku za nyuma.  

Hata kama ni ajira umepata leo haijatokea tu ghafla ukapata utakuta kuna mahusiano uliyajenga siku za nyuma na yamekuletea matokeo hayo siku ya leo.   Kama kuna mteja amekuja kwenye biashara yako leo inawezekana kuna siku za nyuma alisikia au aliona sehemu ikitangazwa.  

Kama unataka wateja wengi kwenye biashara yako siku zijazo tumia nafasi ya leo kuitangaza kwa nguvu au kuwahudumia vyema wateja ulionao sasa hivi. Matokeo ya aina yeyote unayoyataka yanaletwa na matendo madogo madogo unayofanya kila siku.

Hivyo kama unataka matokeo makubwa usichoke kufanya bila kuchoka kila siku.   Hakuna jasho litakalopotea bure kama unalitolea sehemu sahihi. Kama sehemu unayotolea jasho na kufanya kazi kwa bidi ni sehemu sahihi nakwambia haupotezi muda.  

Soma: Hivi ndio Vinakukwamisha  

Hakikisha kila iitwapo leo kuna jambo umefanya ili kutengeneza baadae yako. Leo ndio nafasi ya pekee ya kufanya jambo lolote unalotaka litokee kwenye maisha yako. Jiulize leo Unafanya  nini?  

Karibu sana.

Jacob Mushi

Entrepreneur & Author

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading