Kama maisha yako hayasogei mbele kwa maana ya maendeleo lazima kuna tatizo lipo sehemu. Na siku zote kama maisha hayasongi mbele kuna siku yataanza kurudi nyuma yaani utaanza kuporomoka ka usiporekebisha mapema.

Yapo mambo mengi tofauti tofauti yanayowafanya watu wakwame kulingana na tabia za watu binafsi wenyewe. Tabia moja ambayo unatakiwa uitazame kwa makini ni tabia yako ya matumizi ya pesa.

Kama ukiona umeingia kwenye madeni sana ukweli ni kwamba matumizi yako yamezidi kipato unachoingiza. Labda deni lako liwe na sababu nyingine lakini ukweli ndio huo.

Unachotakiwa kufanya jiulize tangu unaamka asubuhi hadi inapokuwa jioni ni watu wangapi umewalipa pesa? Ni kiasi gani kimetoka mfukoni kwako? Ukishajua piga hesabu uangalie na wewe umeingiza kiasi gani siku hiyo. Hata kama sio pesa halisi angalia ni vitu gani umefanya vitakavyokuletea hizo pesa ulizotumia na Zaidi siku za mbeleni. Kama hakuna ulichofanya ni bora sana ukapunguza vitu ambavyo vinachukua pesa kwenye mifuko yako.

Ni bora uonekane wewe ni bahili kuliko ukajifanya unajali sana watu au marafiki mwisho wa siku unaumia wewe mwenyewe. Marafiki zako wanaweza kuwa sababu yaw ewe kutumia pesa hovyo kama unatoka jioni uko na kampani ya marafiki wanaweza kuwa sababu ya wewe kutumia pesa ambazo hukupanga kutumia. Unaogopa kuonekana wewe ni mbahili lakini madeni yakikutesa wale wale marafiki wanaanza kukusema hasa pale unapokwenda kuwakopa.

Funga milango yote inayotoa pesa hovyo mfukoni mwako bila kurudisha au bila umuhimu wowote. Acha kunywa pombe, kama nyumbani kinapikwa chakula achana na vyakula vya kula na marafiki, acha na michepuko (wanaume) unaweza kuwa na mwanamke wa nje anachukua pesa mfukoni mwako halafu unalalamika madeni.

Embu anza leo kuishi maisha ambayo ni ya tofauti. Kama ulishakutana na bilionea yeyote baa akinywa bia hovyo hovyo kama wewe basi endelea. Kama ulishakutana na tajiri yeyote anaekuvutia akila starehe mara kwa mara kama wewe unavyofanya basi endelea tu utamfikia.

Usipoamua kubadilika wewe hakuna anaeweza kuja kukubadilisha. Badilisha njia ambazo zinachukua pesa mfukoni mwako na angalia namna gani unaweza kutengeneza njia mpya za kuingiza pesa mifukoni mwako. Tengeneza milango mipya ya kuleta pesa ndani ya mifuko yako. Waache marafiki wanafiki wanaokuita kwenye starehe peke yake na sio kwenye dili za pesa.

Marafiki wanaokuita weekend ili mkale starehe hao ni wa kuwakimbia haraka sana. Marafiki ambao mar azote wanazungumzia kutumia pesa badala ya kutengeneza pesa hao ni wa kukimbia haraka bila hata kumuuliza mtu.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

2 Responses

  1. Hakika maarifa yakiwa nasi mkuu Tanzania itakua viwango ,asante sana kwa huduma yako hii nzuri Mungu azidi kukuinua bro.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading