Katika Maisha yetu mambo mengi tunayokutana nayo yakatuhamasisha sana iwe ni biashara au fursa mbalimbali. Au wakati mwingine unaweza kushauriwa jambo Fulani.      

Kama utakuwa huna tabia ya kufanya sasa siku zote utakuja kuishia kujuta peke yake. Inwezekana umekutana na jambo ambalo linahitaji uchukue hatua muda huo huo ukaishia kusitsita baadae unakuja kujuta kwa kutokuchukua hatua.  

Jijengee tabia ya kuchukua hatua kwenye kila jambo unalolitaka, bila ya kuchukua hatua hakuna matendo bila ya matendo hakuna matokeo. Jijengee tabia ya kushukuru kwa matokeo madogo madogo unayoyapata kwenye safari yako ya mafanikio. Kama utashindwa kushukuru kwa jambo dogo unalopata hutaweza kushukuru kwa makubwa.  

Jijengee tabia ya kuanza na kidogo ulichonacho, haijalishi una kiwango kikubwa cha pesa ili kuanzia kufanya jambo. Ukianza kidogo unapata nafasi ya kujifunza na kufanya makosa ambayo  hayatakugharimu sana kama ungeanza na kikubwa.  

Jijengeee tabia ya kusema hapana kwenye mambo yasiyo na tija kwenye maisha yako ya sasa na ya baadae. Ukisema hapana nyingi unajipa nafasi ya kutekeleza yale yaliyo na umuhimu kwenye baadae yako.  

Jijengee tabia ya kuheshimu na kujali kazi za wengine kwani zina mchango Fulani kwenye maisha yako kwa namna moja au nyingine. Kama mtu anafanya kazi hata ya kuchoma mahindi na ni halali heshimu na jali. Hata kama ni konda wa daladala anakusaidia wakati mwingine kuwabeba ndugu zako.  

Soma: Hii ni Milango ya Kufunga kwenye maisha yako  

Maisha ni zawadi ambayo tumepewa ishi vizuri ili zawadi hiyo iwe faraja kwenye  maisha yaw engine waliokuzunguka.  

Karibu sana.

Your Partner in Success

Jacob Mushi

Success Motivator, Author & Entrepreneur

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading