HATUA YA 7; Kurudia Rudia.

By | December 21, 2016
Kabla hujasema Haiwezekani umeshajaribu mara ngapi? 
Kabla hujaamua kuacha umefanya kwa Kiwango cha kuridhisha? Umerudia mara ngapi?

Hivi unajua kila mbegu ina muda wake wa kukaa chini? Kama mwaka jana ulipanda mahindi na hukuvuna kabisa Kwasababu ya uhaba wa mvua haiwezi kuwa mwisho wa kupanda mwaka huu.  Utatafuta namna nyingine.
Tabia ya Kurudia Rudia anatakiwa kuwa nayo mtu yeyote anaetaka Mafanikio makubwa. Ukifanya jambo ukakosa matokeo uliyoyatarajia unarudia tena.  Mwisho wa siku utajikuta Umeweza.
Inawezekana unasema wewe hujui hali ninayopitia ndio maana unaona ni rahisi Kurudia. Ukweli ni kwamba haijalishi ni hali gani unapitia au changamoto gani,  kuacha hakukupi matokeo uliyokuwa unayataka.
Rudia kadiri uwezavyo mpaka uone matokeo unayoyataka.
Asikudanganye mtu hakuna Mafanikio makubwa yanayopatikana kirahisi. Ni wewe mwenyewe kuchagua kufanya kwa bidii bila kukata tamaa au uendelee na maisha uliyoyazoea.
Lazima ukubali kujifunza kila siku. Unajifunza kwenye kila unachopitia,  kwa kuona wengine wanafanya nini,  kusoma vitabu,  kuomba ushauri na mengine mengi.
Chagua moja kutokukubali kushindwa au kuendelea kuishi maisha ambayo wengi wameyachagua.
Rudia, Rudia, Rudia hadi utakapoweza.
Karibu sana.

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668/+255 755 192 418
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com,  www.jacobmushi.com
jacobmushi.com.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *