HATUA YA 71: Usikubali Tabia Hii Ikupate….

jacobmushi
2 Min Read
Mojawapo ya kitu kinchowaponza watu wengi kwenye maisha ni kujisahau. Inafika mahali mtu anazoea hali fulani nzuri hadi anafikiri ameshafika au ameshamaliza kumbe bado safari inaendelea.
Hali hii inaweza kuwa kwenye Biashara, Mahusiano, na Maisha kwa ujumla.
Tabia ya kujisahau imewafanya watu wengi sana kushindwa kufikia ndoto zao. Tabia hii pia imewafanya watu wengi kuharibu mahusiano yao.
Unakuta watu walipokuwa wanaanza mahusiano walikuwa wanafanyiana mambo mazuri wee lakini kadiri wanavyozoeana kuna mambo wanayaacha.
Kama kile ulichokuwa unakifanya mwanzoni kwa bidii ndio kilikuletea mafanikio uliyonayo sasa hivi ukijisahau ukapunguza viwango lazima uporomoke.
Kama kuna ladha Fulani ilikua kwenye bidhaa yako na hiyo ndio iliwavuta wateja wengi kwa kipindi unaanza sasa wamekuwa wengi ukaanza kuipunguza hiyo ladha utaanza kuwapoteza wateja wako.
Kama kuna mambo ulikuwa unafanya ndio yakamvutia huyo uliyenae sasa hivi ukimzoea na ukaanza kuacha ujue utampoteza au utaleta mgogoro.
Kama afya uliyonayo sasa hivi ilisababishwa na wewe kula vyakula bora na kufanya mazoezi sasa hivi umeacha kila kitu. Unakula hovyo vyakula visivyofaa unategemea nini? Kuharibu afya yako ndio kinachofata, baada ya hapo utaanza kupata magonjwa.
Unapojisahau kwa mafanikio kidogo unayoyapata ndio unaanza kuporomoka. unasahau kufanya vile vitu vilivyokufikisha ile sehemu uliyopo.
Mafanikio ni kama kupanda Ngazi sasa unapofikia ngazi fulani ukajisahau ukaacha kusonga mbele unategemea nini? Lazima utaporomoka tu.
Anza kujiuliza mwaswali sasa hivi.
Hapa nilipo ndio nilitaka kufika?
Haya ndio mahusiano niliyokuwa nayataka?
Hiki ndio nilichowaahidi wateja wangu wakati naanza biashara?
Nimesimama au nasonga mbele?
Hakikisha kila siku unakuwa bora na kuongezeka. Ubunifu unatakiwa kila mahali sio kwenye biashara tu kwenye kila sekta ya maisha ubora ni muhimu.
Ukuaji unatakiwa uwe kwenye kila sekta ya maisha yako. Mahusiano, afya, biashara, fedha, ufahamu na kila sehemu yako ya maisha.
Kama unafikiri huhitaji tena kukua jiulize kama umeshafika unakokwenda.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
1 Comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading