HATUA YA 73: Kuhitaji na Kutaka…

jacobmushi
2 Min Read
Unahitajika kuamka mapema Asubuhi lakini mwili unataka uendelee kulala.
Uhitajika ule vyakula bora kwa ajili ya afya yako lakini mwili unataka vitu vitamu na virahisi kupatikana.
Katika vitu ambavyo vitatufanya tuishi maisha ya kukwamakwama ni vitu hivi vya kutaka.
Ukishindwa kutambua ni kipi cha muhimu na kipi sio cha muhimu sasa hivi utajikuta unafanya mambo kwa kuwafurahisha wengine.
Maana uliyojipa juu ya mafanikio wakati mwingine inaweza kukutesa kama ilikua ni mbaya. Mfano wewe mafanikio kwako unaona ni kumiliki gari nzuri. Hapa unasahau vitu vya muhimu sana kabla ya gari. Ungehitaji nyumba ya kuishi kwanza lakini kwasababu gari watu ndio wataanza kuiona unataka gari.
Kadiri vitu unavyovitaka vinapokuwa vingi ndio maisha yanaweza kuwa magumu zaidi. Nguo ulizonazo ungeweza kuzivaa bila ya kununua mpya kwa mwaka huu wote lakini kwasababu hutaki uonekane umepitwa na wakati unataka ukanunua kila nguo mpya inayokuja.
Maisha hayaendi kwa kuonyesha watu una nini. Mafanikio ya kweli yanaleta amani ya moyo na akili. Kama huna amani ya moyo au ya akili kuna tatizo mahali.
Badilisha mtazamo wako kuanzia sasa. Weka mbele yale ya muhimu zaidi kwenye maisha yako. Kama dunia nzima ikijua wewe una pesa nyingi halafu moyoni huna raha na hizo pesa haina maana.
Hatufanyi mambo ili kuwaridhisha watu tunafanya ili kupata amani ya moyo. Kama jambo ambalo unalifanya halileti amani ndani yako basi kuna tatizo.
Angalia sana vitu unavyivitaka na vitu unavyovihitaji. Utakuta ndani umejaza vitu sio kwasababu vilikuwa vinahitajika lah! Ni ulitamani tu.
Jiulize!
Ni kweli nakihitaji?
Maisha yangu yatakwama wapi nikikosa hiki kitu?
Je ninapata amani ya ndani?
Sijasema usiwe na vitu vizuri lah! Kila jambo na wakati wake. Jua lipi ni la kuwa nalo sasa hivi na lipi ni la miaka mitano ijayo.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading