Najua utashangaa vipi huyu leo anazungumzia kifo, amepatwa na nini? Lakini nikotoe hofu kwamba hakuna ubaya kabisa kuzungumzia jambo ambalo linalotokea kwenye maisha yetu kila siku.


Ukweli katika jambo ambalo limekuwa gumu sana ni mtu kujua siku yake ya kuondoka hapa duniani. Na hata mwanadamu afikirie kiasi gani sijajua kama atakuja kugundua siku ambayo ataondoka.

Kama huwezi kutatua jambo mara nyingi tunashauri uachane nalo. Lakini pale jambo lile linapokuwa linagusa maisha yako kila siku lazima utafute namna ya kulitazama mara ya pili.

Kwasababu ya kifo watu wengi wamekuwa wavivu na kuacha kufanya mambo makubwa wakisema “yote tutayaacha hapa duniani” ndio ni kweli yote utayaacha lakini ni vyema ukaacha msingi mkubwa kwa ajili wengine.
Wengi wamekuwa na hofu sana wanapofikiria juu ya suala la kifo. Nataka leo ubadilishe hofu hiyo iwe hamasa kwako. Embu kiangalie yaangalie maisha kama ofa Fulani ambayo itakwisha baada ya muda, hivyo hutachezea ovyo muda wako hapa duniani. Yatazame maisha kama kifurushi ambacho baada ya muda Fulani kitakwisha muda wake wa matumizi halafu kitumie kifurushi hicho kwa mambo mema hapa duniani.

Unapofikiria kuhusu kifo chako iwe sababu yaw ewe kuongeza kasi kwenye kuliishi na kulitimiza kusudi la wewe kuwa hapa duniani.

Unapofikiria kifo chako badala ya kupata hofu anza kufanya yale mambo ambayo unafikiri ukiondoka utakuja kujutia sana kama hukuyafanya.

Unapofikiria juu ya kifo ondoa woga kabisa anza kutazama maisha yako yote uliokwisha ishi hapa duniani uangalie ni umbali kiasi gani umefika na ni umbali kiasi gani umebakiza.


Hukuzaliwa kwa bahati mbaya na usikubali kuondoka bila kuacha alama hapa duniani. Ondoa mashaka na hofu kwani kufa utakufa tu angalia kile unachokifanya usikiache nusu.

Kuna watu wanapowaza maisha yao kwamba kuna siku watakufa wanajiambia kwamba sasa hizi mali nazitafuta za nini wakati nitaziacha? Ndio utaziacha lakini jiulize wewe umeshatumia za wangapi waliocha? Kama na wao wangekuwa wabinafsi kama wewe wakasema waondoke bila kufanya chochote dunia isingekua hapa ilipo sasa hivi.

Jipatie kitabu Nilichoandika Kiitwacho Siri 7 za Kuwa Hai Leo piga simu 0654726668.

Jacob Mushi.
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com.

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading