Katika zama hizi ubunifu wako ndio unakutoa. Haijalishi unauza bidhaa iliyokuwepo miaka 20 iliyopita lakini ukiwa mbunifu unaweza kuleta mapinduzi.
Watu wengi hadi zama hizi wanaendesha biashara au mambo yao kwa njia zile zile za miaka kumi iliyopita halafu anategemea mabadiliko.
Huwezi kupata matokeo tofauti kama hufanyi vitu vya tofauti. Kuna msemo unasema “ukitaka kupata kitu ambacho hujawahi kukipata basi fanya kitu ambacho hujawahi kukifanya” hivyo basi ni muhimu kujua ni matokeo ya aina gani tunataka na ni hatua zipi tuchukue.
Dunia ya sasa inabadilika kwa kasi kutoka analogia kwenda digitali hivyo kwa chochote unachokifanya jaribu kukitazama katika namna ya tofauti. Jaribu kufikiri namna ya kukihamisha kwenda Digitali.
Kama utakuwa unafanya biashara kwa mifumo ile ile ya zamani kamwe usitegemee matokeo ya tofauti. Kaa chini uangalie ni namna gani biashara yangu inakwenda kwenye mfumo wa digitali.
Na hapa kikubwa ni kuangalia njia gani ya kumpata mteja wako katika mifumo mipya ya digitali.
Biashara ya kukaa mahali unamsubiri mteja aje umwonyeshe bei ilishapitwa na wakati. Lazima ukubali kufanya kitu cha ziada na tofauti na wengine. Nafikiri hata nyani ukimfundisha vizuri anaweza kusimama mahali akaelekeza watu bei.
Jaribu leo kaa chini kwenye chochote unachokifanya angali unahamiaje digitali?
Unahitaji kuwa na vitu vichache tu.
Mitandao ya kijamii na tovuti ya biashara yako. Kifaa ni hichi hichi unachosomea kila siku.
Kupata tovuti ya biashara yako tuwasiliane.
Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
E-mail: jacob@jacobmushi.com
Blog: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading