Uadilifu ni kitu cha muhimu sana kwenye Maisha yetu ili kutuwezesha kujenga historia nzuri. Watu wengi wanakosa uadilifu ndio maana biashara zao zinakufa baada ya muda mfupi. Uadilifu ni sifa ambayo itakufungulia milango mingi ya fursa huko mbeleni.
Kama utakosa uadilifu katika hatua hizi za mwanzo unaanza kuonyesha picha ya wewe ulivyo na  huko mbeleni utakavyokuwa. Watu wataogopa kukupa vitu vyao au pesa zao ufanyie kazi kama huna uadilifu.
Jinsi unavyozungumza na watu.
Unazungumza vipi na watu unaokutana nao? Kwani kila mtu anakutafsiri tofauti jaribu kutafuta maneno ambayo hayataleta tafsiri mbaya kwenye akili za watu. Kuna namna unaweza kuongea watu wakaona unaringa au una dharau. Kuwa makini sana.
Matendo yako kwa wengine,
Unawatendea nini wengine? Je wewe utafurahia ukitendewa hayo? Jaribi kurekebisha na hili. Maana ipo siku na wewe utakuwa kwenye nafasi ya kutendewa utapenda utendewe yale uliyowatendea wengine?
Unapokuwa peke yako wafanya nini?
Mara nyingi tunapokuwa peke yetu ndio tunaonyesha tabia nyingi mbovu tunazozificha mbele za watu. Jaribu kutafakari sasa ni jambo gani la siri huwa unapenda kulifanya? Je watu wakigundua itakuwaje? Utabakia salama?
Zingatia Haya:
Kuwa Muwazi kwenye mambo yako. Angalia sana usiwe una mambo unayaficha na yanahitajika yajulikane na watu iwe bosi wako au wafanyakazi wako. Ipo siku utakosa namna ya kusema mbele za watu.
Kuwa mkweli usiwe na mambo ambayo hayaeleweki yaani hata wewe mwenyewe huwezi kuyaelezea.
Kuwa mwaminifu, usitapeli, usitamani pesa usiyoitolea jasho.
Uadilifu ndio utafanya mafanikio yako yadumu na uzidi kukua kuelekea juu Zaidi.

 

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading