Kuna wakati unaweza kupitia magumu sana kwenye dunia hii ukadhani upo mwenyewe. Kuna wakati ukadhani mbona ni wewe tu yanakukuta? Najua ulishwahi kujiuliza mambo kama haya.
Ukweli ni kwamba lolote unalopitia sasa hivi sio jipya sana. Karibu kila unalopitia kuna wengine walipitia eneo japo mazingira na baadhi ya vitu vinaweza visifanane lakini kuna mambo huwa yanaingiliana.
Haupo mwenyewe kwenye changamoto unayopitia sikwambii hivi ili ujisahau kwamba unatakiwa utoke uendelee mbele na safari. Nataka kukutia moyo pale unapojiwa na hisia kwamba ni wewe peke yako unapitia hayo.
Raha ya changamoto huwa hazimwonei mtu. Yaani haiwezekani likalokupata ikawa ni kwa kukuonea lazima kuna chanzo ambacho kimesababisha.
Ndio unaweza ukasema mbona nilichongewa na wafanyakazi wenzangu nikafukuzwa kazi? Ndio lakini kuna kitu kilikuwa nyuma ya wao kukuchongea. Yapo makubwa yanatokea sio kwamba ni watu wanaonewa bali ndio asili ya dunia ilivyo.
Changamoto ndio asili ya Maisha hapa duniani.
Nikutie moyo kwamba sehemu unayopita sasa hivi usikubali ikuache hivi hivi. Hakikisha unatoka ukiwa mtu mpya, ulieongezeka ufahamu wa kutatua makubwa Zaidi ya hilo lililokwisha.
Soma: Kitu Cha Thamani ni Hiki
Una uwezo mkubwa sana na nguvu kubwa ipo ndani yako ya kukuwezesha kufanya makubwa na kuzivuka changamoto. Mnyama anaeliwa nyama porini angelalamika kwa kusema dunia haiko sawa kwanini nilizaliwa kitoweo cha wengine unafikiri ingekuwaje?
Unaweza kupiga hatua nyingine kubwa Zaidi japo unapotia magumu kiasi gani nafasi bado unayo.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com