Moja wapo Ya vitu vinavyowavuta watu kwako Zaidi ni kupitia kitendo cha kutabasamu. Watu wengi wamejikuta wakiingizwa mtegoni kwa kuvutwa na tabasamu.

Wengine wamevutwa na tabasamu wakajikuta wamenunua vitu wasivyovipenda.

Wengine wamevutwa na tabasamu hadi sasa ni wagonjwa na wanajutia sana na kulalamika tabasamu la yule kaka ndio lililonifikisha hapa.
Wapo pia waliofikia mafanikio makubwa na kutimiza ndoto zao kwa kupitia tabasamu hilo hilo.

Wewe unavutwa na nini?
“Kuna siku moja nilikuwa natembea maeneo ya mjini huku nina kiasi cha pesa mfukoni ghafla nikapita mbele ya duka zuri la nguo nikavutiwa na bidhaa zao nikaingia ndani kutazama. Ukweli wakati naondoka nyumbani asubuhi sikupanga kununua chochote lakini kwa kupitia tabasamu la mhudumu yule nikajikuta nimenunua nguo.”

Kila mmoja ana hadithi Fulani ambayo anaikumbuka ilishamtokea kwa kusababishwa na tabasamu. Inawezekana wewe ndiye uliyetabasamu ukampata mtu au kuna mtu alitabasamu akakupata.

Leo nataka ujiongeze sasa kwasababu naamini unacho kitu unafanya na kinawagusa watu. Anza leo kutumia tabasamu lako kuwavuta wengi waje waone au wasikie kile unachokifanya. Unapomuelezea mtu jambo unalofanya kamwe usisahau kutabasamu.

Watu ambao nina uhakika wanatakiwa wafanye biashara yao wakiwa wana huzuni ni wauza majeneza na misalaba peke yao.

Biashara nyingine kutabasamu ni muhimu sana kwani ndio njia ya kwanz aya kumfanya mteja aendelee kuja kila wakati.


Haijalishi umeamka katika mazingira ya aina gani kwamwe usionyeshe mbele ya mteja wako. Haijalishi biashara imekuwa ngumu kiasi gani usikubali kuonyesha hasira au masikitiko mbele ya unaemhudumia.

Kawaida kila binadamu anapenda kufanyiwa mambo mazuri na kuonyeshwa kuwa anajaliwa hivyo ukiweza kutumia njia hii utaweza kupata unachokitaka.

Kutabasamu sio kwenye biashara pekee kwenye chochote kingine unachokifanya usiache kuonyesha uso wenye furaha. Hii inamfanya unaemhudumia aone wewe mwenyewe unapenda kile unachokifanya.

Japo kuwa unapitia matatizo mengi lakini kutabasamu iwe ndio salamu ya kwanza kabla hujatamka neon lolote kwa mgeni anaekuja mbele yako.

Kila kitu kikitumika vizuri kinaweza kuleta mabadiliko makubwa kwenye Maisha yetu.

Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
jacobmushi.com

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *