Chochote unachotaka kukikamilisha kwenye ulimwengu wa nje lazima uanze kukikamilisha katika ulimwengu wako wa ndani. Yaani lazima uanze kupata picha ya kitu hicho katika ulimwengu wako wa ndani ambao ni fikra zako.
Kama unataka kufikia ushindi kwenye kitu chochote unachokifanya lazima uanze kushinda ndani ya akili yako. Kama akili yako inasitasita basi ujue utasumbuka sana kwenye utekelezaji.


Chagua Kushinda kwanza ndani ya akili ndipo uanze kuchukua hatua. Unapochagua kushinda nadni ya akili yako unakuwa umeviambia vikwazo vyote kwamba hakuna wa kunizuia kufikia ushindi.

Usikubali chochote kikukwamishe haijalishi changamoto zitakuwa kubwa kiasi gani lakini kama umechagua kushinda huwezi kukubali kukwamishwa na chochote kwenye dunia hii. Vikwazo vipo vingi lakini wewe pekee ndio unakubali viwe sababu ya kushindwa kwako.

Kama hujachagua kushinda moja kwa moja unakuwa umechagua kushindwa. Hili unatakiwa ulitambua kwamba kama hujachagua kushinda basi tayari umechagua kushindwa. Kama akili yako haijaona ushindi basi ujue ukikutana na vikwazo unashindwa kuendelea mbele. Anza ushindi wa ndani ndipo ushindi wa nje uonekane.

Nimekuwa najifunza sana kwa watu kupitia vitu mbalimbali vya kila siku. Kitu kimoja nimegundua ni kwamba huwezi kumsaidia mtu kufanya kile anachotakiwa kukifanya yeye binafsi ndio anatakiwa afanye maamuzi kutoka ndani. Kama mtu hajaamua kujitoa ili afikie ushindi kwenye jambo analolitaka hata siku moja hawezi kufikia kwa kuhamasishwa ndio maana ni muhimu sana wewe mwenyewe uanze kufanya kitu kinachotoka ndani yako.


Unapoanza na kitu kinachotoka ndani yako na ukadhamiria kabisa kufikia ushindi ndipo nafasi ya kuhamasishwa inapatikana. Kama jambo unalolifanya ulisikia tu mahali kwamba linalipa au ulisoma mahali ukahamasika basi ni rahisi sana kuja kuacha.

Anza na ushindi kila siku asubuhi. Chagua kitu kimoja ambacho utakuwa unakitekeleza kila siku ili ufikie ndoto yako. Kama huna kitu unachokifanya kila siku ili kufikia maono yako basi unapoteza muda hapa kila siku.
Your Partner in Success
Jacob Mushi
Success Motivator, Author & Entrepreneur
Phone: +255 654 726 668
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading