Kitu kingine kinachowafanya watu waishie kutapatapa kwenye Maisha haya ni kutokujua au kusahau kule wanapokwenda. Ukishindwa kujua kule unapoelekea utajikuta Maisha yako yanaendeshwa na kile unachokiona sasa hivi kwa Maisha ya kawaida.
Kujua unapokwenda ni kwa kuanza kufahamu lengo kuu la Maisha yako hapa duniani. Unapofahamu lengo hili unatengeneza maono yako makubwa juu ya lengo lako kuu.
Lengo kuu la Maisha yako pamoja na maono makubwa ndio yanakupa mwongozo wa nini cha kufanya, na hatua gani uzichukue kila siku.
Watu wengi wamekuwa wakiongozwa na Maisha ya wengine. Mtu nafanya jambo sio kwasababu linalenga kwenye lengo kuu la Maisha yake bali kwasababu ameona wengine wanafanya.
Ni kweli tunahitaji kuwa na nyumba nzuri za kuishi, magari mazuri, kwenda kutembea sehemu mbalimbali za dunia lakini haya ni malengo ya kawaida sana ya Maisha. Kwanza yanakugusa wewe peke yako.
Badala ya kutumia nguvu nyingi kuwaza juu ya vile vitu ambavyo vinayagusa Maisha yako mwenyewe anza kuwaza kwenye vitu vinavyogusa Maisha ya watu wengi. Unapogusa Maisha ya wengi unakuwa umegusa na vile vitu vyako vyote vidogo vidogo vya kawaida.
Soma: Upendo ni Kupoteza
Maisha mazuri sio kutembelea gari la bei ghali kuliko wengine. Maisha mazuri sio kuishi kwenye nyumba ya kisasa kuliko wengine. Hivyo unavyoviona vya kisasa sasa hivi baada ya miaka michache vitakuwa vya kawaida sana. Maisha mazuri ni kuishi kwa kulitimiza lengo kuu la Maisha yetu.
Mtu mwenye Maisha mazuri ni yule anaelitimiza lengo la Maisha yake kila siku.
Hakikisha umetambua lengo Kuu la Masha yako.
Jiunge na semina kubwa sana inyofanyika mwezi wa nne kwa kiingilio kidogo sana. Tuma neno semina kwenda namba 0654726668.
Jacob Mushi

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading