Connect with us

HATUA YA 92: Kubali Kwamba Hujui…

HATUA ZA MAFANIKIO

HATUA YA 92: Kubali Kwamba Hujui…

Ili uweze kujifunza mambo mengi Zaidi lazima uanze kukubali kwamba hujui chochote. Hata kama una vitu vingi sana ndani ya kichwa chako bado una vitu vya kujifunza kwa wengine. Jambo linawafanya watu wabakie na vile vitu wanavyovijua pekee ni pale mtu anapojiona sasa tayari ameshajua kila kitu. Au mtu anapojiona sasa yeye ameshakuwa mtu hawezi […]

Ili uweze kujifunza mambo mengi Zaidi lazima uanze kukubali kwamba hujui chochote. Hata kama una vitu vingi sana ndani ya kichwa chako bado una vitu vya kujifunza kwa wengine.

Jambo linawafanya watu wabakie na vile vitu wanavyovijua pekee ni pale mtu anapojiona sasa tayari ameshajua kila kitu. Au mtu anapojiona sasa yeye ameshakuwa mtu hawezi kuonywa tena na wazazi wake.
Kama ukishindwa kutambua kwamba kila siku mpya kuna kitu kipya unatakiwa ujifunze kwa wengine utajikuta husongi mbele. Wakati mwingine ukijiona hakuna hata mmoja anaekukosoa inabidi uanze kujiuliza maswali.
Huenda umeshapotea kuna watu wameona haushauriki hivyo wameamua wakuache tu hadi utambue mwenyewe kwamba unakosea. Au basi unafanya vizuri. Ni muhimu sana kujiuliza mara kwa mara kama njia unayopitia ni sahihi.
Mithali 14: 12 –  Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu,Lakini mwisho wakeni njia za mauti. ..
Kuna mambo unaweza kuwa unayafanya na ukajiona upo sahihi sanalakini kumbe unapotea bila kujua. Kubali kuonywa kubali kukaripiwa, kubali kwamba unakosea kwa kujua au bila kujua. Mpende sana yule anaekuonyesha makosa yako maana hapendi upotee.
Kama ukifika mahali ukaanza kujiona upo sahihi kwenye kila unalolifanya, hata kama ni kweli upo sahihi kitendo cha kujiona upo sahihi ni makosa. Yaani haupo sahihi kujiona upo sahihi.

Hii ni kwasababu ukishajiona upo sahihi huwezi kujifunza kitu kipya wala hakuna mtu mwingine ataweza kukwambia kitu ukamwelewa kwasababu unajiona upo sahihi.


Usijione wewe mwenyewe kuwa mwenye hekima;mche Mwenyezi-Mungu na kujiepusha na uovu (Methali 3:7)


Sisemi hivi ili wewe ujidharau na kujiona kwamba unakosea bali ni ili kuruhusu watu wanaokuona waweze kukushauri na kukurekebisha. Kuna makosa unaweza kuyafanya ukiwa uwanjani usioyaone lakini wanaokuangalia kwa nje wanaweza kukushauri vizuri zaidi.


Maisha ya hapa duniani ni ya kwako ndio lakini lakini lazima ukubali kuna watu walishapita hapo unapopitia. kama utashindwa kufuata kanuni na nidhamu zinazotakiwa lazima uanguke.
Mpumbavu peke yake ndie anadhani anajua kila kitu. Lakini mwerevu hukubali kujifunza na kuonywa katika njia zake.
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza Hapa

Jipatie Vitabu Hapa…. 

Jiunge na semina kwa njia ya mtandao tuma majina yako na neno semina kwenda namba 0654726668.

Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: 0654726668
jacobmushi.com
Continue Reading
You may also like...

Jacob Mushi ni Mwandishi wa makala, nukuu na vitabu vya Maisha na Mafanikio, Kocha wa Maisha na Mjasiriamali. Kiu yake kubwa ni kuona wewe unakuwa mtu bora, unatimiza ndoto zako na unaishi Maisha ya mafanikio. Kazi yake kubwa ni kuhakikisha wewe hauishii Njiani kwenye lile kusudi ambalo Mungu ameweka ndani yako.

Click to comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

More in HATUA ZA MAFANIKIO

To Top