Tulipokuwa shuleni tulikuwa na mwalimu wa nidhamu. Kazi ya mwalimu huyu alikuwa anahakikisha tunakuwa na tabia ambazo haziwezi kuleta uharibifu shuleni. Hata kama shule iwe ni ya watu wa aina gani lazima kitengo cha nidhamu kiwepo.

Ukija kwenye uaskari na jeshini vilevile kuna vitengo vya nidhamu. Lengo la vitengo hivi ni kwa ajili kuhakikisha watu wanakuwa na aina ya Maisha ambayo ndio yanatakiwa kwenye eneo husika.
Bahati mbaya sana katika Maisha yetu ya kawaida hakuna mwalimu wa nidhamu wala hakuna kitengo hicho. Kuna umri ukishafikisha ukatoka nyumbani unapoishi  unakuwa unaishi Maisha ambayo unayataka mwenyewe.
Kwa kukosekana mtu ambaye anatusimamia ndipo mtu huamua kufanya jambo ambalo anaona kwake ni sahihi. Kwa kukosekana kwa mtu wa kututazama ndipo hujichanganya na makundi ambayo hayafai. Mwingine anaweza kufikiri labda shuleni alikuwa anaonewa au nyumbani sasa ndio yuko huru.
Sasa mtu akishakosa nidhamu anajikuta anaishi Maisha ya hovyo sana. Kwasababu bila nidhamu binafsi kwenye Maisha yako unashindwa kudhibiti baadhi ya mambo ambayo yanaendelea hapa duniani. Duniani kuna mambo mengi yanafanyika yanaweza kuwa sahihi au sio sahihi lakini sio kila jambo ambalo linanafanywa ufanye wewe.
Ukosefu wa nidhamu umewaharibu vijana wengi sana. Unakuta mtu anajiachia kiasi ambacho lolte ambalo linawezza kutokea linamkuta.
Nidhamu ina mambo mengi mapana sana lakini kwenye Maisha ya kawaida ukishindwa kujiwekea nidhamu unakosa Maisha ambayo ni bora nay a kuigwa kwenye jamii. Bahati mbaya sana hakuna mtu wa kukuchapa tena. Kuna vituo vya polisi lakini kule wanapekwa wakosefu wa nidhamu waliopindukia.
Anza leo kujiwekea nidhamu na misngi ya Maisha yako mwenyewe. Sio kwasababu unataka kumridhisha Fulani au dini yako bali ni kwasababu umeamua kuishi hivyo. Bila nidhamu ya Maisha kila janga linakuja litakuchukua.
Unaweza kuona wazazi wakikufuatilia wanakunyima uhuru lakini ni kwamba wanataka uishi Maisha ambayo ni bora. Unaweza ukawadharau ukafikiri labda ni wazee wa zamani wanaleta Maisha ya zamani lakini kumbe unapotea.
Jijengee nidhamu kwenye chochote unachokifanya. Hapo ndipo unaweza kuishi vizuri. Jitahidi uweze kudhibiti hisia zako na vitu vidogo ambavyo vinakuleta raha ya muda mfupi.

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza Hapa

Jipatie Vitabu Hapa…. 

Jipatie Kitabu cha Siri 7 za Kuwa Hai nitafute kwa namba 0654726668.

Jiunge na semina kwa njia ya mtandao tuma majina yako na neno semina kwenda namba 0654726668.

Karibu sana.
Jacob Mushi
Entrepreneur & Author
Phone: +255 654 726 668
Email: jacob@jacobmushi.com
Blogs: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading