Mara nyingi wanadamu tunatafuta vitu kwa nguvu kubwa sana. Huku tukiwa na mawazo kwamba baada ya kuvipata tutavifurahia sana.

Kitu cha ajabu ni kwamba baada ya kuvipata tulivyokuwa tunavitafuta tunaanza kuona kama vile havitoshi tena. Tunaanza kuhamisha tena mawazo yetu kwenye vitu vingine ambavyo hatuna kisha tunaanza kuvitafuta tena.

Hali hii imekuwa sababu ya watu kuishi maisha yasiyo na furaha na ukosefu wa amani na utulivu kabisa.
Watu wengi wananunua nguo nzuri, wanakuwa na wapenzi au wenzi wazuri na wanasahau tena thamani yao na kuanza kuona mapungufu yao.

Hali hii inasababisha watu kuachana kwenye mahusiano au hata kwenye ndoa. Pia inasababisha kutokujali kabisa vile vitu tulivyo navyo.

Ili usije ukaishi maisha yako yote ukiwa unatafuta, wapenzi wapya, magari mengine, na vitu mbalimbali lazima ujijengee tabia ya kuthamini kile ulichonacho sasa hivi.

Kile ulichonacho sasa hivi ndio kinakuweka mjini, haijalishi ni kibaya au unakionaje wewe lakini bila ya hicho ungekuwa kwenye hali mbaya zaidi.

Kaa chini utafakari kama ungekuwa huna huyo mtu ulienae sasa maisha yako yangekuwaje? Kama ungekosa hizo nguo ulizonazo ungekuwa na maisha ya aina gani?

Ungepoteza kila kitu ambacho unacho sasa hivi maisha yako yangekuwa magumu sana.

Maana yangu hapa sio kwamba turidhike na tulivyo navyo laah! Maana ni tuvipe thamani vitu tulivyomavyo sasa hivi ili tuishi maisha ya furaha tukiendelea kuboresha maisha yetu zaidi.

Usije ukapotelea kwenye kutafuta ukasahau kwamba kuna ambavyo unavyo tayari. Siku vikiondoka ndio utagundua thamani yake.

Karibu Sana

Jiunge na Semina kubwa Kwa Njia ya Mtandao. Gharama nafuu Tsh elfu Tano. Tuma neno Semina kwenye namba 0654726668.

Jacob Mushi
Author &Entrepreneur
Phone: 0654726668
E-mail: jacob@jacobmushi.com
Website: www.jacobmushi.com
jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading