HATUA YA 96: Jitafute Mwenyewe Kwanza.

jacobmushi
2 Min Read
Kama bado hujajitafuta na kutambua wewe ni nani huwezi kujua watu wapi ni sahihi kwenye Maisha yako. Kazi ya kwanza ambayo unapaswa kuanza kuifanya ni kujitafuta wewe mwenyewe.

 

Maisha ya watu wengi yamekuwa magumu sana kwasababu walianza kutafuta watu Fulani kwenye Maisha yao kabla hawajajitafuta wao. Kama hujajitambua wewe ni nani utakuwa ni mtu wa kila mtu.
Watu wengi wamekosa mwelekeo wa Maisha na kujikuta hawajui ni nini cha kufanya kwasababu hawajajitambua wao ni kina nani. Kila linalotokea mbele yao ni sahihi.
Watu wengine wameishia kufanya kazi ambazo hawazifurahii kila wakati wanaendelea kuumia mioyo kwasababu waliruka hatua ya kwanza ya kujitafuta. Kama ulipata kazi kwa kushauriwa ukafanye na mtu Fulani huwezi kuifurahia kazi hiyo. Labda na wewe uwe uliipenda kutoka moyoni.
Kama umeshindwa kujitafuta na kujitambua wewe ni nani huwezi jua ni wapi unakwenda. Huwezi kujua ni watu gani wakuambatana nao. Huwezi kujua ni vitabu gani unatakiwa usome. Huwezi kujua safari yako ni ngumu kiasi gani na itachukua muda kiasi gani.
Kujitafuta sio zoezi la siku moja inahitaji kuchukua hatua za mara kwa mara hadi utambue wewe ni nani. Inahitaji kukaa peke yako muda mwingi na kutafakari juu ya Maisha.
Soma: Kitabu Siri 7 Za Kuwa Hai Leo
Lazima ukubali kujitoa na kukaa sehemu peke yako utafakari juu ya Maisha yako. Katika kufikiria juu yakow ewe mwenyewe utaanza kupata majibu. Fikiria kwa kujiuliza maswali mbalimbali juu ya aina ya Maisha unayoyataka. Sehemu gani unataka kufika, kwanini upo duniani na mengine  mengi.
Ukiweza kujitafuta na kujitambua utajua unatafuta nini hapa duniani. Watu wengi tumejipoteza au tupoteza ule uhalisia wetu kwasababu ya mambo mengi ya dunia hii yanayovutia pamoja na ushauri wa watu.

Rafiki Yako,

Mwandishi na Kocha wa Mafanikio

Jacob Mushi

www.jacobmushi.com/huduma

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading