Biashara nyingi zinazoendeshwa mara nyingi mwenye biashara lengo lake ni apate pesa tu. Kama wewe una mtazamo wa aina hii kwenye biashara utachukua muda mrefu sana kufikia mafanikio au kukua zaidi ya hapo ulipo.

Ni kweli pesa inahitajika ili biashara ikue. Ni kweli bila pesa hakuna biashara. Lakini sasa kama wewe utakuwa unatazama pesa tu utakuwa unakosea sana.
Lazima ukubali kubadili mtazamo wa biashara yako. Badala ya kuangalia pesa angalia kwamba wewe unatatua matatizo ya watu. Na ukishatatua matatizo ya watu wanakulipa.
Mara nyingi ukipanda kwenye daladala, ni mara chache sana ukakutana na kondakta ambaye anakubali kupata hasara hata mara moja. Hii inatokana na mtazamo wake kwenye biashara anayoifanya. Wengi wamejisahau hawajui kuwa wapo kwenye biashara.
Hawawezi kuongea vizuri na wateja wao. Hawakubali hata siku moja wapokee pesa pungufu au wamsamehe mtu asilipe. Mara nyingi wao hulalamika na kugombana na wateja wao.
Wakati unapanda utabembelezwa ukishakaa kushuka ni ugomvi, kurudishiwa chenchi ni ugomvi. Wanasahau majukumu yao ni kutafuta chenchi kwa ajili ya wateja wao.
Sasa kwa haya ambayo makondakta hufanya hua yapo pia kwenye biashara zetu za kawaida. Watu hawajui kwanini wapo kwenye biashara.
Mara nyingi inaweza kusababishwa na aliejiriwa hana mafunzo ya kutosha au sababu nyingine yeyote.
Kama wewe hujawahi kukubali hata siku moja upate hasara kwasababu ya makosa yako kwa mteja upo sehemu ya hatari sana.


Kama wewe siku zote unaangalia faida yako tu. Na hujawahi kutazama mteja wako ameridhika  hata siku moja huwezi kukua.
Lengo kuu liwe ni kutatua tatizo la mteja sio wewe kupata pesa. Kama utatatua tatizo vizuri utalipwa zaidi.
Ni bora usimuuzie kitu mteja kuliko ukamuuzia akaenda kulalamikia bidhaa yako.
Kubali kupata Hasara mara moja moja. Ili biashara ijenge jina.
Jipatie Kitabu Siri 7 za  Kuwa Hai Leo wasiliana nami kwa 0654726668.
Jacob Mushi
Author &Entrepreneur
Phone 0654726668
E-mail: jacob@jacobmushi.com

Blog: www.jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading