HATUA YA 99: Kitu Gani Kinakutambulisha?

Swali ambalo ukiulizwa unatakiwa ujibu bila ya kusitasita ni kitu gani kinakutambulisha wewe? Kama utaishi hapa duniani na ukatambulika kwa jina lako au mzazi wa Fulani ni sawa hujaishi.    

Hakikisha kuna kitu kinakutambulisha wewe hapa duniani nah ii ndio inaleta furaha ya kweli. Sizungumzii kuwa maarufu Lah! Unaweza kuwa unafanya kazi ya kawaida sana ambayo wengine wanaidharau lakini imetoka ndani yako na ikakufanya ukawa mtu mkuu siku moja.  

Ni jukumu lako kuanza kugundua kitu cha kukutambulisha. Haijalishi una umri gani sasa hivi bado una nafasi ya kukaa chini na kugundua.   Makosa makubwa ambayo utayafanya na utakuja kujutia siku ukiondoka hapa duniani ni kutokufanya lile lililokuleta hapa duniani.  

Maisha yako yanabebwa na kile kinachokutambulisha. Kama huna kinachokutambulisha basi huna Maisha hapa duniani.  

Amua sasa kuchukua hatua leo, usiendelee kupoteza muda kufanya mambo mengine ambayo hufurahii. Ni kujitesa sana na kutojitendea haki kabisa kufanya mambo ya kawaida na ambayo hayatoki ndani ya moyo wako.  

Nikushauri jambo moja ndugu yangu hakikisha umetambua leo upo duniani kwa kusudi lipi Maisha yako yataanza kuwa na Amani na furaha.   Haimaanishi ukitambua kusudi lako hutapitia changamoto hapana, changamoto utazipitia lakini kule unakotaka kufika utafika endapo hutakata tamaa.  

Soma: Kubali Kujinyima  

Wako wengi wanakuwa na shauku kubwa sana ya kufanya mambo mbalimbali lakini wanaishia njiani baada ya kukutana na changamoto Fulani. Kamwe usiwe mtu wa wa kuacha kufanya jambo kwasababu ya changamoto.    

Jacob Mushi

Entrepreneur & Author

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading