Tumejifunza kuhusu mafanikio na utajiri lakini hivi havitatokea kama huna vitu ambavyo unavifanya kila siku vinavyokuvuta kwenye mafanikio na utajiri. Leo tunakwend kuangalia mambo kadhaa ya kufanya ili ufikie kwenye kilele cha mafanikio.

1.  Jifunze vitu chanya vitakavyokuza ufahamu wako kila siku angalau kwa dakika 30. Angalau kwa siku tenga muda wa dakika 30 wa kujifunza na kuongeza ufahamu wako. Hii itakusaidia sana uweze kua mtu makini.
2.  Pangilia siku inayofuata kabla hujalala. Kabla hujalala hakikisha umeshajua ratiba yako nzima ya kesho utaenda kufanya nini. Andika vitu vyote unavyokwenda kufanya siku inayofuata,
3.  Sikiliza audio books (vitabu vilivyosomwa). Hii unaweza kufanya unapokua unatembea njiani, kwenye gari yako au hata ukiwa nyumbani umepumzika.
4.  Punguza au acha kabisa kufuatilia habari. Kuna tatizo kubwa ambalo tunalo kipindi hichi ambalo ni la taarifa. Kipindi hichi habari zipo nyingi sana mara sijui nani katumbuliwa, mara nani kaficha sukari, sijui nani kafanyaje. Kama huna utatuzi wowote kwenye habari mbaya unazozifuatilia achana nazo. Jifunze kuchagua nini cha kuweka kwenye akili yako.
5.  Achana na umbea kusema watu vibaya. Zungumza vitu chanya juu ya watu wengine. Kama huna jambo lolote zuri la kusema juu ya mtu ni bora ukakaa kimya. Hakikisha unachowaambiwa wengine kuhusu mtu Fulani unaweza kukizungumza wakati nay eye akiwepo pia.
6.  Jiiunze tabia ya kushukuru kila siku hakikisha una kitu cha kushukuru kila siku. Unaweza kutazama vile vitu ulivyo navyo halafu utengeneze picha ukiwa huna utakua kwenye hali gani. Kisha mshukuru sana Mungu.
7.  Hudhuria semina na mafundisho mbalimbali. Hii itakusaidia wewe ukutane na watu mbalimbali watakaoweza kua na msaada au wewe kujifunza mambo mengi kutoka kwao.
8.  Jifunze kusikiliza wengine. Shida kubwa tuliyonayo kipindi hiki tuna watu wengi ambao hawawezi kuwasikiliza wengine. Jifunze tabia hii ya kusikiliza wengine na kuwaelewa itakuwezesha ujenge mahusiano mazuri na kila mtu.
9.  Fanyia kazi malengo yako kila siku hakikisha haipiti siku hujafanya chochote kinachokupeleka wewe kutimiza malengo yako.
10.  Hakikisha umefanya jambo jema kwa mtu kila siku. Yaani kila siku jifunze kuwatendea wengine mambo mema. Tenda wema utalipwa mema.
11.  Tenga muda wa kukaa na uwapendao. Wanaweza kua marafiki, familia, mke/mume, mchumba. Hata kama upo bize kiasi gani tenga muda wako tu kama wako mbali angalau hata dakika 5 uzungumze na mtu kwenye simu.
12.  Tabasamu. Kua mtu wa tabasamu ukitabasamu unavutia mambo mengi mazuri na watu chanya watakufuata. Jaribu kununu siku moja kisha nenda sehemu yenye watu jichanganye nao ukiwa umenuna hivyo hivyo uone siku yako itakavyokua.
Asante sana kwa kufuatana name. Ukiweka kwenye vitendo haya uliyojifunza utaona matokeo yake. Na usisite kunitumia maoni yako au ushauri kwa mawasiliano hapo chini.
Jacob Mushi
Mawasiliano 0654726668 Email jacob@jacobmushi.com yako.

Rafiki yako  Jacob Mushi
Mawasiliano 0654726668 Email jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading