MAISHA NA MAHUSIANO

485; Unafikiri Kwanini Utahukumiwa Wakati Hukuja Duniani Kwa Maamuzi Yako?

on

Leo nakumbuka siku yangu ya kuzaliwa, nimetimiza miaka kadhaa hapa duniani. Katika kutafakari mambo mbalimbali na kujiuliza maswali nilijikuta katika mawazo haya, “Mimi sijawahi kumuomba Mungu aniumbe binadamu, sasa inakuaje nikikosea ameahidi adhabu mbalimbali?” kwanini niadhibiwe kwa Maisha ambayo hata sijayachagua kuishi?

Ukweli ukitafakari hayo maneno yako kama yana ukweli Fulani ndani yake. Lakini hupaswi kuishia hapo katika tafakari yako unapaswa uendelee kuchimba ndani Zaidi.

Mimi pia sikuishia hapo, katika kutafakari nikajikuta nawaza tena, hivi ni aina gani ya mifugo huwa inatuomba tuiofuge? Paka alishawahi kuomba afugwe na binadamu? Je mbwa? Kuku? Mbuzi bata? Nikaja kugundua kumbe hii mifugo pia haijawahi kuomba kufugwa nasi, ni sisi wenyewe tuliafanya maamuzi ya kuwafuga kutokana na uhitaji wetu.

Hivyo basi endapo paka ataharibu kitu huwa tunamuadhibu, mbwa akimuuma mtoto lazima apigwe kipigo cha uhakika, vivyo hivo Wanyama wengine. Sasa tujiulize yeye Mungu sio zadi ya sisi binadamu? Kama tunaweza kuwaadhibu Wanyama hata kufikia kuwaua kwasababu ya makossa mbalimbali na Wanyama hao hawajawahi kuja kutuomba tuishi nao iweje kwa Mungu tushangae?

Hapo ndipo nikapata majibu ya kwamba lazima tukubali kuishi vile Mungu anataka tuishi na tukikaidi basi tusimlaumu kwa lolote baya litakalokuja juu yetu. Kama ambavyo Wanyama hupata adhabu mbalimbali hata kwa majirani ndivyo kwa upande Fulani Maisha yetu yako hivyo.

Tuendelee kumpenda Mungu, kutenda yaliyo mema, kuwapenda wanadamu wenzetu na kuishi vizuri. Ni kweli hukuomba kuumbwa lakini hupaswi kuishi utakavyo kwasababu upo kwenye dunia yenye mwenyewe. Yeye alieiumba dunia anataka uishi hapa duniani vile anavyotaka yeye na sio vile unavyojiamulia wewe.

Nakutakia kila la Kheri katika Kutimiza mapenzi ya Mungu Wako.

Rafiki Yako Jacob Mushi.

www.jacobmushi.com

About jacobmushi

Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

12 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published.