Watu wengi wamekuwa waoga hasa pale wanapojilinganisha na wengine na kujiona wao ni wa kawaida na hivyo kushindwa kujitambulisha vyema wanapokutana na wengine.
Unaweza kufanya makossa ukapoteza wateja wapya ambao ungewapata kwa kusema tu unachokifanya, hata kama huna ofisi usiogope kusema unafanya biashara gani.
Kuwa Mfuasi wa Kwanza wa Ndoto zako, usisubiri hadi watu waanze kusemea kazi zako kwamba ni nzuri jiamini na unapokutana na mtu jitambulishe bila woga kwa kusema kile unachokifanya.
Unaposema bila kuogopa na watu wanaamini na watachagua kuwa wateja wako. Usiogope kwa kujilinganisha na wengine ambao wameshakupita.
Sema vile Unavyotaka Watu wajue Kuhusu wewe, ila tu usiseme ambavyo Sio vya Kweli wasije wakatarajia makubwa wakayakosa.
Jiunge Nasi Hapa… Bonyeza Maandishi haya
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
“Piga Hatua”