Unapokuwa na Ndoto kubwa na shauku ya kwenda kuitimiza kuna watu wengi sana wanaweza kujitokeza kwenye Maisha yako kama washauri na wenye maoni yao juu ya kile unachotaka kufanya. Watu hawa wanaweza kuwa marafiki wa karibu na ndugu zako wa damu kabisa.

Wote hawa wanaweza kutoa maoni yao juu ya kile unachokifanya kwa namna mbalimbali. Kuna ambao watakwambia achana na hizo Ndoto kabisa huwezi kufanikiwa, wengine watakushauri kitu kingine cha kwenda kufanya. Wewe binafsi kulingana na unavyowafahamu unaweza usiwaelewe kama wanakukatisha tamaa kweli au ni wana maana gani kukwambia hivyo.

Sasa unatakiwa uwaelewe kuwa wapo wa aina Mbili:

Wanaokujali;

Hawa wanaweza kuwa watu wako wa karibu sana, kwasababu ya woga wao na namna wanavyofikiri wao wanaweza kuwaza kushindwa wanakuonea huruma hivyo wanakosa namna ya kufanya Zaidi ya kukwambia uache.

Mfano unaweza kuwa na mzazi ambaye anataka usomee masomo Fulani na hataki kabisa ujihusishe na kipaji chako. Yeye binafsi ana amini huwezi kufanikiwa kwenye kipaji chako bali unaweza kuwa na Maisha mazuri endapo utasoma.

Mzazi kama huyu sio rahisi akuelewe hata kidogo kama yeye ndio anahusika na kila kitu kwenye Maisha yako. Hapa inahitajika nguvu ya ziada kumwelewesha akuelewe.

Wenye Wivu;

Hawa wanaweza pia kuwa ndugu zako au marafiki zako na lengo lao ni wewe usifanikiwe kuwazidi wao. Siku zote watanena mabaya kwenye kile unachokifanya. Hawa ni rahisi kuwaelewa kama sio watu wa karibu sana na wewe unajua tu huyu ana wivu. Lakini kama ni mtu wa karibu inaweza kuwa ngumu sana kujua kama ana wivu au ni anakujali tu.

Unachopaswa Kufanya:

Siku zote usipende kuwa muwazi sana kwa watu ambao hawana Ndoto kubwa kama zako. Haijalishi ni ndugu zako wa karibu kama unajua hawa watu wanaweza kuwa sababu ya kunirudisha nyuma usiwaeleze kila jambo. Hakikisha unawafahamu vizuri marafiki zako ili unapokuwa kwenye mazungumzo ujue ni kipi cha kumwambia huyu na kipi sio cha huyu.

Pili hakikisha unatoka kwenye Maisha ya utegemezi kwa watu. Unapokuwa na watu ambao unawategemea kwa asilimia kubwa wanaweza kuyaendesha Maisha yako. Utakuwa huna maamuzi juu ya kile unachokitaka.

Hatma yako ni yako usikubali mtu mwingine yeyote aje ayavuruge Maisha yako kwasababu tu ya maoni yake. Ni bora mara mia kutengana na watu kuliko kupotea kwenye Maisha yako.

 

Nakutakia Kila la Kheri,

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading