Vile unavyojiona ndani yako ndio kunafanya uwe mtu unaejiamini au mwoga. Kunafanya pia uwe mtu unaethubutu kuchukua Hatua au uwe mtu wa kusitasita na kuahirisha.

Namna unavyojiona ndani yako kunaweza kuathiriwa na namna ulivyokuwa tangu ukiwa mdogo. Yale maneno ambayo ulikuwa unaambiwa mara kwa mara yanaweza kuwa sababu ya jinsi unavyojiona sasa.

Vilevile unaweza kujiona wewe huwezi kutokana na namna unavyojilinganisha na wengine. Kama utawatazama watu ambao umesoma nao au wenye umri kama wako ukaona wameshakupita kimafanikio unaweza kuanza kuwa na picha mbaya juu yako.

Unatakiwa kutengeneza picha nzuri ndani yako kabla hata ya wengine kuwa na picha nzuri juu yako. Ukikosa picha nzuri juu yako unaweza kuwa mtu wa kushindwa kila unalolifanya. Unakosa kujiamini hata unashindwa kuwa na matokeo mazuri kwenye mambo yako.

Ulishawahi kuona jambo moja linafanywa na watu wawili tofauti  lakini mmoja anafanya vizuri Zaidi na mwingine anafanya vibaya kabisa lakini wote wanauwezo mzuri kabisa? Hii inatokana na namna ya mtu anavyojiona ndani yake.

Kuna mambo mengi unashindwa sio kwasababu ni magumu bali ni kwasababu wewe unajiona kama mtu alieshindwa kabla hata hujaanza kufanya. Maana yake unakuwa umeshindwa kabla hata hujachukua Hatua.

Anza kubadilisha picha uliyonayo juu yako.

Jione wewe ni mshindi bila ya kujalisha umeshafanya kitu gani au lah.

Jione ukiwa umefikia zile Ndoto zako kubwa.

Acha kabisa kusema maneno mabaya juu yako, siku zote jinenee vile ambavyo unataka kuwa. Jisemee yale ambayo unataka kuona yanatokea kwenye Maisha yako huku ukiyaweka kwenye vitendo.

Maisha yako yatabadilika kama utaanza kubadili picha yako ya ndani.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Nakutakia Jioni Njema.

Rafiki Yako.

 

Jacob Mushi,

Author | Trainer | Entrepreneur

Simu: 0654 726 668 |0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Facebook:  Jacob Mushi 

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading