#HEKIMA YA JIONI; Dunia Haijawahi Kuwa Sawa na Haitaweza Kuwa Sawa.

jacobmushi
2 Min Read

Kwenye dunia hii haijawahi kutokea hata siku moja kukiwa na idadi kubwa ya watu na watu wote wakawa wanafurahi tu bila matatizo ya aina yeyote. Kuna mambo mengine yanatokea ni mabaya ndio lakini ni kwasababu ya mazuri ambayo yanapaswa kutokea mahali Fulani.

Wewe unapovuna mazao mengi shambani na ukapeleka sokoni ukiwa na matumaini ya kupata faida kubwa unaweza kukutana na bei ipo chini. Kwako itakuwa ni maumivu lakini kwa wengine ni furaha.

Kuna nyakati wewe unafurahia mafanikio yako kumbe kwa kupitia kile ulichokipata wewe kuna wengine wanaumia. Haina maana kwamba kuna kuumia ili wengine wafurahi lakini kuna baadhi ya mambo lazima iwe hivyo. Mkulima hawezi kufurahia bei ghali ya mazao yake sokoni bila ya watu kuumia kwa kununua kwa bei ghali.

Kuna watu wengine watatakiwa waumie ili wewe upite sehemu Fulani. Kuna nyakati zinatokea mtu mwingine anapoteza kazi yake ili wewe upate kazi.

Unapofurahi unatakiwa ukumbuke kuna mtu mahali anaumia. Hii itakusaidia wewe kuweza kuwa na adabu katika matumizi ya kile ulichokipata.

Ukiweza kutambua hilo yanapokuja mabaya kwenye Maisha yako huwezi kuwa mtu wa kulalamika kwasababu ndio dunia ipo hivyo. Hatuwezi kufurahi siku zote lazima kuna nyakati za ugumu ili kupisha mambo mengine mazuri Zaidi.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Jacob Mushi,

Author, Entrepreneur, Trainer, Life Coach,

Simu: 0654 726 668/0755192418,

Twitter:  @jacobmushitz

Instagram: @jacobmushi

Facebook:  Jacob Mushi 

Barua pepe: jacob@jacobmushi.com

TAGGED:
Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading