Maisha ya mwindaji na mfugaji yanaweza kuwa mfano mzuri sana kwenye Maisha yetu ya kila siku na kama tutaweza kuwatazama vizuri watu hawa tunaweza kujua tupo upande upi.

Mwindaji.

Mtu wa aina hii siku zote anatumia nguvu Zaidi katika matendo yake. Ili aweze kuwinda lazima atumie nguvu zake.

Mtu wa aina hii anawaza Zaidi kula leo kuliko siku za mbeleni kwasababu yeye anawinda ili ale leo haafu kesho atakwenda tena kuwinda.

Ni mara chache sana atatumia akili ni hasa pale tu mnyama anapomsumbua wakati wa kumkata au kumwinda na mshale wake.

Mwindaji anafanya kazi kwa bidii sana lakini anaishia kula yale matokeo ya kazi yake siku hiyo hiyo.

 

Mfugaji;

Mtu huyu sifa yake kubwa anafuga na kuzalisha kile anachokifuga hivyo kinaongezeka.

Mtu huyu anawaza Maisha ya baadae kwasababu kwa kupitia mifugo yake ataweza kuishi miaka mingi ijayo bila ya kufanya kazi kubwa sana.

Mfugaji anatumia akili Zaidi kuliko nguvu zake za mwili.

 

Watu hawa wawili ukiwaletea mnyama alie hai mbele yao kila mtu atamtazama mnyama kwa namna yake. Mwindaji atawaza kitoweo na mfugaji atawaza huu ni mfugo ambao utazalisha Wanyama wengine Zaidi.

Wewe unazionaje fursa zinapokuja mbele yako? Unaweza kuwa mtu anaetazama fursa kama mwindaji, mtu anaewaza kupata dili la pesa na kisha akatafute sehemu nyingine. Lazima ubadili mtazamo wako katika fursa zinazokuja mbele yako. Lazima uwaze katika namna ya kukua na kuongezeka, kwani hapo ndipo kwenye mafanikio.

 

Ukiwaona hawa wawili unaweza kusema mwindaji anafanya kazi kwa bidi kuliko mfugaji. Lakini kufanya kazi kwa bidii peke yake haitoshi lazima ujue namna ya kuzalisha kile unachokifanyia kazi ili kiongozeke na kukufanyia kazi. Ukweli ni kwamba mtu pekee anaeweza kuja kuwa na Maisha yenye mafanikio Zaidi ya mwenzake ni mfugaji kwasababu yeye anatunza na kuzalisha Zaidi kile anachokifuga. Mwindaji yeye akiona windo anawaza kuuua na kuchinja, itampasa awinde kila wakati ili aweze kuishi.

 

Nataka ujiulize kwa kile unachokifanya kila siku je wewe umekuwa upande gani?

Umekuwa ni mtu anaefanya kazi na kula yale matokeo ya kazi yako yote?

Je una mpango gani na Maisha yako ya baadae?

Nguvu zako unazotumia sasa hivi kufanya kazi kwa bidii zikiisha utakuwa kwenye hali gani?

 

Lazima uweze kubadilisha mtazamo wako, kufanya kazi kwa bidii peke yake haitoshi lazima ufikiri katika namna ya kukuza kile unachokifanyia kazi ili uweze kuishi Maisha ya uhuru. Lazima uwaze katika namna ya kutengeneza mfumo ambao utakuwezesha uendelee kutengeneza kipato hata kama hautakuwa na nguvu za kutosha kuendelea kufanya kazi kama sasa.

Badili Mtazamo wako na Utabadili Maisha yako.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading