Wanadamu tumezoea kuongea sana, hasa kwa maneno tunayoyasikia kwa wengine.

Ukweli ni kwamba maneno mengi ambayo tunaambiwa na wengine hatuna uhakika nayo kwa 100%.

Hivyo basi lolote unaloambiwa juu ya mtu kama huna uhakika baki nalo moyoni mwako.

Mara zote penda kujiuliza ni faida gani utaipata kwa kusema hayo maneno. Kama hakuna faida ambayo unapata basi hakuna haja ya kusema.

Maneno haya ninayozungumzia ni yale ambayo mtu anakuja kukwambia fulani kafanya hivi na hivi.
Maneno kama hayo na watu wa aina hiyo ni wa kukaa nao mbali kabisa.

Ili uishi maisha yenye furaha na mafanikio wekeza muda wako kwenye mambo yanayokujenga wewe na wengine.

Achana na Umbea, Udaku, na mengine yote yasiyofaa.

Ni mimi Rafiki Yako.
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
Piga Hatua Timiza Ndoto Yako.
www.jacobmushi.com

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading