Kulikuwa na kijana mmoja alikuwa anataka mafanikio sana. Akamfuata Mentor wake na kumuomba amuelekeze ili na yeye aweze kufanikiwa. Mentor wake akamwambia kesho tukutane ufukweni mwa bahari asubuhi.
Yule kijana akajisemea moyoni mwake, “mimi nataka mafanikio na pesa lakini ameniambia tukutane ufukweni kwani nimemuomba anifundishe kuogelea?” akasema tena, “kwa vile nataka pesa na mafanikio nitakwenda.”
Kesho yake akafika asubuhi na mapema pale ufukweni akakuta na mentor wake ameshafika tayari. Mentor wake akamshika mkono na akamwambia tuanze kuingia ndani ya maji. Kadiri walivyoingia ndani ya maji walizidi kusogea chini Zaidi na maji kuwafikia karibu na vifua vyao.
Mentor wake kwa ghafla sana akamzamisha ndani ya maji kwa nguvu bila ya yeye kutarajia. Kijana yule akabaki akitapatapa kwenye maji kwa nguvu sana huku akirusha mikono huku na kule. Alipochoka kabisa ndipo mentor wake akamtoa ndani ya maji.
Akamuuliza swali moja,” Ulipokuwa ndani ya maji ni kitu gani ulikuwa unakitaka?” kijana akajibu, “nilikuwa nataka kupumua”
Mentor wake akamjibu,” Kama Ukiyataka mafanikio kama ambavyo ulikuwa unataka kupumua ndani ya maji kwa hakika utayapata”
Tunajifunza nini kwenye mfano huu?
Watu wengi wanasema wanataka mafanikio lakini ile shauku ya kuyataka mafanikio hayo sio kubwa kiasi cha kuwafanya wachukue Hatua yeyote ile halali ili waweze kuyapata.
Ni wengi sana wanaweza kusema kwamba wanataka vitu Fulani kwenye Maisha yao lakini ni wachache wanaweza kuchukua Hatua.
Ni wengi sana wanaweza kuongea sana juu ya Ndoto zao lakini ni wachache wanaweza kuanza kufanya mambo yanayowaletea matokeo hata kama ni kidogo kwenye Ndoto zao.
Amua sasa kuchukua Hatua ili uweze kuifanya Ndoto yako iwe kweli.
Shauku yako ya kutaka mafanikio, inatakiwa iwe kubwa kama mtu alie jangwani bila tone la maji. Kiwango cha uhitaji wako wa mafanikio ndio kitaamua ni ukubwa wa Hatua kiasi gani utachukua kila siku.
Chukua Hatua Timiza Ndoto Yako.
Ni mimi Rafiki Yako,
Jacob Mushi
USIISHIE NJIANI
Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.
Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA
Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/