#HEKIMA YA JIONI: Kuchukua Hatua.

Hatuhitaji watu wengi wanaoweza kulielezea jambo Fulani vizuri bali tunahitaji watu wachache wanaoweza kuchukua Hatua juu ya jambo husika. Tuna upungufu wa watu wanaochukua Hatua ndio maana hatuna maendeleo.

 

Badala ya kuendelea kuongea maneno matupu fanya kile kilichopo kwenye uwezo wako kwanza. Kwa kupitia hicho ndio utaona uwezekano wa kufanya makubwa Zaidi.

Tuna wengi wanabakia kusema ningekuwa na hiki ningefanya hiki na kile, sasa badala ya kungojea hicho hiki jiangalie una nini au unaweza kufanya nini uanze. Kuna njia nyingine utaziona ukishafuata ile njia ndogo iliyopo mbele yako.

 

Kwa kuchukua Hatua moja kutakufanya uone njia nyingine Zaidi za kukuwezesha kufika kwenye Ndoto yako.

Kama unaweza kuandika andika, usisubiri sijui hadi ufike wapi.

Kama unaweza kuimba imba sasa hivi usingojee kitu kingine.

Chukua Hatua kwa kile ambacho kipo kwenye uwezo wako na utaona njia nyingine mbele yako. Aliepewa talanta moja kati ya wale wengine watatu alitakiwa kuitumia talanta moja kuzalisha na sio kuangalia wengine walipewa nyingi.

 

Hutahukumiwa kwa kufanya kidogo bali utahukumiwa kwa kutokutumia hata kile kidogo ulichopewa. Acha kuwatazama wengine na kusema ningekuwa kama Fulani ningefanya hivi na hivi au ningekuwa nimefika mbali angalia kile ulichowezeshwa nacho na uchukue Hatua.

Acha kuendelea kusubiri wakati Fulani ufike, huenda ulitakiwa uishi Maisha ya ujana tu hapa duniani na wewe kwa kutokutambua hilo ukabaki unasubiri tu hadi kifo chako kitakukuta ukiwa hujafanya chochote.

 

Ninapowatazama vijana wadogo wakifariki naumia sana na kuwatazama wale waliokuwa wakiniambia unaandika wewe umefanya kitu gani hadi watu wasome unachoandika? Kwasababu huenda Mungu anataka ufanye jambo Fulani mapema kwasababu anajua hutakuwepo hadi huo muda wa kufanya makubwa ambayo wengine wanataka ufanye.

Usikubali Ndoto yako ife kwa kusikiliza maneno ya wengine ambao hawajui hata kwanini unafanya unachokifanya.

Fanya kile kilichopo kwenye uwezo wako ili uweze kufungua uwezekano mwingine zadi.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

https://jacobmushi.com/

jacobmushi
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading