#HEKIMA YA JIONI: Kusudi la Mungu na Kusudi La Mwanadamu.

jacobmushi
3 Min Read

Mungu ametuumba na akatuleta duniani kwa makusudi yake yeye mwenyewe. Pamoja na hayo bado kuna watu ambao hawajaweza kutambua makusudi ya wao kuwepo hapa duniani. Niliwahi kusema kwamba chanzo cha maovu mengi yanayoendelea hapa duniani ni kutokana na watu wengi kuishi Maisha ambayo sio ya kwao yaani kutokutambua kwanini wapo hapa duniani.

Mungu hajakuumba uje duniani kuua wanadamu wenzako, Mungu hajakuumba uje usababishe watu waishi kwa hofu na mashaka hapa duniani. Ukiona wewe watu wanakuogopa kuliko wanavyomwogopa Mungu basi ujue hujatumwa na Mungu.

 

Ukiona unaweka mbele Zaidi matakwa yako kuliko kuyagusa Maisha ya wengine ujue upo nje ya mpango wa Mungu. Huwezi kulazimisha watu wakubali kile ambacho Mungu amekuleta uje kukifanya ila kwa kukifanya watu wakaona matokeo yake huanza kukubali.

 

Watu wengi wanafanya mambo kwasababu tu ya tamaa za Maisha ambayo wanataka kuishi na hivyo kuwasahau kama wengine ni binadamu. Ukishaweka kusudi lako mbele ya kusudi la Mungu lazima uwe unaumiza Maisha ya wengine.

 

Penda kujiuliza maswali sana hasa pale unapoona unachokifanya kinawaumiza watu badala ya kuwafanya wafurahie uwepo wako hapa duniani. Jiulize maswali ni kweli Mungu alikutuma au ni tamaa zako mwenyewe.

Bahati mbaya Mungu hakulazimishi umfuate yeye bali anaweza kukuonya  kwa kupitia watu wake. Mwisho wa kusudi lilitoka nje ya kusudi la Mungu huwa ni uharibifu, na uharibifu wa mwisho unakuwa ni mbaya sana kwasababu unamgusa yule alikuwa analitimiza lile kusudi la mwanadamu.

 

Ukiona tamaa inazidi sana kwenye maamuzi yako ujue umeshaanza kwenda nje ya kusudi la Mungu.

Jiulize leo upo hapa duniani kuumiza watu au kufanya Maisha ya wengine yawe bora?

Kama ni hivyo kwanini watu wanalia kwasababu yako?

Mwisho wa mpango ulio kinyume na mpango wa Mungu huwa ni uharibifu mkubwa. Mwisho wako utakuwa mbaya sana endapo utakuwa umeliasi kusudu la Mungu.

 

Kile unachokifanya penda kujiuliza mara kwa mara je bado nipo kwenye mstari? Bado nipo ndani ya kusudi la Mungu? Unaweza kujikuta umeshatoka nje  ya kusudi na unavutwa na tamaa zako mwenyewe. Na hapo hata ukiambiwa husikii unaona watu wanakuonea wivu.

Nakupenda Sana Rafiki Yangu , Natamani Uliishi Kusudi La Mungu.

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

 

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

 

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading