Uking’atwa na nyoka wakati mwingine ukiguswa na majani tu unaweza kushtuka na kudhani ni nyoka tena. Inapotokea umepatwa na changamoto uanatakiwa usikubali ziwe sababu ya wewe kuendelea kutembea ukiwa na umakini wa hali ya juu kiasi kwamba ukasahau kutazama kule unakotaka kufika.

 

Unaweza kuingia kwenye biashara ukapata hasara kubwa kiasi kwamba ukaishia kuwa mtu wa hofu tu yaani kila wazo linalokuja la kufanyia kazi unaogopa kupoteza pesa.

Unaweza kuwa na mahusiano ambayo yalikuumiza kiasi kwamba ukaishia kuwa mtu wa tahadhari tu na kuogopa kuumizwa kila wakati.

 

Mambo mabaya yaliyowahi kutokea kwenye Maisha yako usikubali kuyapa nafasi ya kukufanya wewe ushindwe kuendelea kufuhia Maisha yako.

Unachotakiwa tu ni wewe kujifunza ili usirudie tena, kuishi kwa thadhari na kuogopa kila unapoguswa na jani kunakufanya ukose furaha ya Maisha. Kuna mambo utashindwa kuyafanya kwa ufanisi kwasababu ya hofu ambayo imekuingia .

 

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading