Siku zote nafasi iliyoachwa wazi ndio inatumika kwa mabaya au mazuri.

Kukiwa kuna nafasi iliyoachwa wazi kwenye mahusiano inaweza kusababisha mahusiano kuvunjika endapo atatokea mtu na kujua namna ya kuitumia vyema nafasi hiyo.

Nafasi iliyoachwa wazi kwenye biashara inaweza kuwa sababu ya wewe kushindwa kibiashara na mshindani wako endapo ataamua kuitumia vyema na kwa wateja ambao wanakuja kwake na kwako.

Nafasi iliyoachwa wazi kwenye Maisha yako inaweza kuwa sababu ya wewe kuingiliwa na vitu ambavyo havikutakiwa.

 

Nafasi iliyoachwa wazi inaweza kuwa, ni udhaifu wako, uzembe wako, au sehemu ambayo unaipuuzia na kuona ni kawaida.

Jifunze kutumia nafasi ambazo zimeachwa wazi kwenye Maisha yako ili kujiokoa na matatizo yanayoweza kutokea.

 

Ndoa nyingi zimevunjika kwasababu ya watu kushindwa kujua ni wapi kuna uwazi umebaki.

Biashara nyingi zimekufa kwasababu kuna nafasi nyingi ziliachwa wazi washindani wakazitumia.

 

Wahenga wanasema “usipoziba ufa utajenga ukuta” ufa ni kama nafasi iliyoachwa wazi, isipozibwa inaweza kusababisha matatizo makubwa Zaidi.

 

Usingoje mpaka ya kukute siku zote jitahidi kuangalia ni sehemu gani ambayo inapaswa kuziribwa mapema.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading