#HEKIMA YA JIONI: Shuka Chini.

jacobmushi
2 Min Read

Kuna nyakati ukitaka kupanda juu Zaidi ya wengine lazima ukubali kushuka chini. Unakubali kuonekana mtumwa kwa siku chache ili uweze kupata yale ambayo yatafanya Maisha yako ya badae yabadilike kabisa.

 Kushuka chini na kunyenyekea haimaniishi ufanye mambo ya hovyo ambayo yanaondoa utu wako bali ni ukubali kufanya mambo halali haijalishi yanaonekana ni ya hadhi ya chini kiasi gani.

Kubali kuonekana mdogo lakini kumbe unajifunza yaliyo makubwa Zaidi.

 

Biblia inasema kuwa ukitaka kuwa mkubwa kuliko wengine lazima ukubali kuwa mtumishi wao. Yaani unapowatumikia watu ndipo unainuliwa na kuwa juu.

 Watu wengi tunapenda kuanza kuwa juu kabla ya kuanza kutumika. Watumikie watu utainuliwa juu na kila mmoja atalijua jina lako.

Katika kujishusha chini kuna mambo unaweza kupitia ukafikiri unaonewa kumbe ni kwa ajili ya kukufunza na kukutengeneza uwe imara. Endelea kujishusha.

 

Nyenyekea, Mheshimu Kila Mtu, Tenda Wema kwa kila mtu. Unapoyafanya haya ni kwa faida yako wewe mwenyewe. Hiyo faida unaweza usiione leo lakini ukaja kuiona miaka kadhaa ijayo.

Ni mimi Rafiki Yako,

Jacob Mushi

USIISHIE NJIANI

Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.

Jipatie Vitabu vya Biashara na Mafanikio Hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Tengeneza Kipato kwa kupitia Blog Bonyeza hapa.. BONYEZA MAANDISHI HAYA

Karibu Kwenye Kundi Maalumu la WhatsApp https://jacobmushi.com/whatsapp/

Share This Article
Follow:
Jacob Mushi is a Tanzanian Author, Minister, Entrepreneur, Founder and CEO of NETPOA.
Leave a comment

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading