Kuna mambo ambayo yanaweza kukutesa na kukusumbua sana kwenye maisha yako. Kuna mengine yanakuwa mzigo mzito sana ndani yako.
Kuna mahali unafika unajisikia kuchoka kabisa na unakuwa umekata tamaa kabisa. Kutokana na ugumu wa mambo mengine wengine hufikia maamuzi ya kutaka kujiua.
Neno langu kwako leo ni kwamba usichoke, kuna mambo hata pesa haiwezi kuwa suluhisho.
Kuna mengine akili zote za wanadamu hufikia kikomo.
Ukishajua jambo unalopitia halipo kwenye uwezo wa mwanadamu unapaswa kumwendea Mungu mwenyewe. Mpelekee matatizo yako ambayo wanadamu na fedha zimeshindwa kutatua.
Yeye hujitokeza siku zote pale ambapo tunakuwa tumefikia mwisho wa akili zetu.
Mkabidhi yeye atakuonyesha njia.
Usijichoshe wala kujitesa kwa kuumia na kuwaza sana. Yupo anaeweza yote. Akili zako zinaposhindwa yeye atakuonyesha njia.
Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/