Habari Rafiki, Leo ni siku nyingine tena ambayo tumepewa kama zawadi kwa ajili ya kwenda kuyafanya Maisha yetu yawe bora Zaidi.

Jisemeshe Maneno Haya Kabla Hujatoka Kwenda kufanya Chochote.

“NACHUKUA HATUA, NAJIFUNZA, NAWEKA JUHUDI NA BIDII, NAVUMILIA.
MAFANIKIO NI HAKI YANGU, EEH MUNGU NIWEZESHE.”

Mambo mengine yanakuwa magumu kwasababu mtazamo wako unavuta ugumu. Inakupasa kutengeneza mtazamo wa kushinda kwenye yale mambo unayofanya.

Mtazamo wa kushindwa ndio unawakwamisha watu wengi na kuwafanya waogope kujaribu. Mtu anaanza kuona kushindwa ndani yake kabla hajachukua hatua yeyote.

Wapo watu ambao wanaweza Kukutengenezea mtazamo wa kishindi na kushindwa. Watu hawa ni wale ambao umewaamini sana na kuwapa nafasi ya kuwasikiliza.
Wakisema jambo fulani haliwezekani hata kama ulikuwa una hamasa kubwa kiasi gani unajikuta umekubali kushuka chini na kuwasikiliza.

Kaa na watu ambao wanakutia moyo na kukueleza ukweli, watu ambao wameshajaribu mambo makubwa zaidi yako. Ukikaa na watu ambao hawajawahi kufanya chochote kikubwa yaani wewe kwao ndio umefanya makubwa zaidi utajikuta wanakukatisha tamaa.

Marafiki waliokwisha kufanya makubwa zaidi yako watakuambia jambo fulani usifanye hivi fanya hivi na wala hawatakukatisha tamaa. Wanaweza wakakwambia hili usifanye sasa hivi anza na hili kwanza. Hivyo unapaswa kuwaelewa pia pale wanapokupa ushauri.

Tengeneza mtazamo wa kushinda ili uweze kupambana na changamoto unazopitia kila siku.

Ni mimi Rafiki Yako, Jacob Mushi
#UsiishieNjiani
“Piga Hatua, Timiza Ndoto Yako.”
https://jacobmushi.com/patavitabu/

Andika Maoni Yako Hapa

Discover more from Jacob Mushi

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading